
DAVID
Moyes ameendelea kufagia njia ya Manchester United kuelekea kukosa
nafasi ya kushiriki michuano ya UEFA msimu ujao baada ya kupigwa mabao
2-0 dhidi ya Everton katika dimba la Goodison Park usiku huu.
Mabao ya Everton yalifungwa na Leighton Baines dakika ya 28 kwa mkwaju wa penati na la pili lilifungwa na Kevin Mirallas katika dakika ya 43.
Moyes alishindwa kutazama mechi hiyo baada ya kuona timu yake ya zamani ikimwadhibu Goodison Park.
Matokoe ya leo ni dalili ya Moyes kumaliza ligi nje ya timu nne za juu.
Wakati
huo huo, Moyes amelazimika kutumia mkutano wa baada ya mechi na
waandishi wa habari kufafanua hatima ya mshambuliaji wake Danny Welbeck
ambaye anaripotiwa kuihama klabu hiyo msimu huu.
Moyes alieleza kuwa taarifa za Welbeck kutaka kuondoka Old Trafford ni uzushi tu na hana mpango wa kumuondoa.
Vyombo vya habari leo asubuhi viliripoti kuwa Welbeck aliyeanzia benchi katika mechi ya leo anaweza kuihama klabu yake hiyo.
“Danny Welbeck ni mchezaji muhimu kwangu na namthamini sana. Ni muhimu kwa Manchester United”.
Kipigo cha leo kinaashiria Man United itakosa Champions League msimu ujao, lakini Moyes amewashukuru mashabiki walio sambamba na timu katika msimu huu mgumu kwao.
“Mashabiki wamekuwa nyuma yetu na kututia moyo wakati wote”.
“ Wanatambua kuwa msimu ni mgumu kwetu na nadhani wameisapoti timu, lakini wanaelewa kuwa mambo si mazuri” Alisema Moyes.
0 comments:
Post a Comment