
Na Baraka Mpenja, Dar Es Salaam
MABINGWA
Azam fc wanatarajia kuandika historia hapo kesho kwa kutwaaa taji bila
kupoteza mechi yoyote ambapo watakabiliana na JKT Ruvu katika uwanja wa
Azam Complex, Uliopo Chamazi, nje kidogo ya jijini la Dar es salaam.
Hii itakuwa mechi ya mwisho kwa Azam fc waliocheza mechi 25 mpaka sasa bila kufungwa.
Kocha
mkuu wa klabu hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog alisema kutwaa
ubingwa ni mafanikio makubwa, lakini kuchukua mwari bila kufungwa mechi
yoyote ni historia nzuri kwa klabu.
“Wachezaji
wangu wasibweteke na ubingwa. Bado tuna mechi moja kesho dhidi ya JKT
Ruvu. Nahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka rekodi nzuri”.
“Tutaingia kwa nguvu zote na kuhakikisha tunawafunga wapinzani wetu”. Alisema Omog.
Naye kocha mkuu wa JKT Ruvu Fredy Minziro alisema kikosi chake kimejiandaa kukabiliana na Azam fc kwa nguvu.
“Tunafahamu kuwa Azam fc ni timu bora msimu huu. Hajafungwa mechi yoyote na wanahitaji kujenga historia kupitia sisi”.
“Tumejiandaa
vizuri na kizuri ni kuwa tumenusurika kushuka daraja. Nilishasema toka
awali kuwa malengo yetu ilikuwa kukwepa kushuka daraja na hivi sasa
tumeweza. Tunamshukuru Mungu na tunamuomba atuongoze vyema hapo kesho”.
Alisema Minziro.
Msimu
huu umekuwa mzuri mno kwa Azam fc kwani toka mzunguko wa kwanza
walicheza kwa mafanikio wakiwa chini ya kocha mkuu, Sterwat John Hall.
Baada
ya Hall kujiuzulu mwishoni mwa mzunguko wa kwanza, Mcameroon Omog
alichukua nafasi yake na kuendeleza rekodi ya kutofungwa.
JKT Ruvu wapo nafasi ya 9 kwa pointi 31 baada ya kucheza mechi 25, hivyo wapo mikono salama kabisa.
Azam
fc wamecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 59 kileleni, huku tayari
wakiwa mabingwa kwasababu hakuna klabu yoyote inayoweza kuzifikia pointi
hizo.
0 comments:
Post a Comment