Na
Baraka Mpenja, Dar Es Salaam
0712461976
YANGA
SC wenye machungu ya kupoteza ubingwa wao msimu huu baada ya kuwasili jana jioni
kutoka Arusha wameamua kutuliza akili yao katika hoteli ya Landmark, Kunduchi,
jijini Dar es Salaam ili kujiwinda dhidi ya Simba sc jumamosi uwanja wa Taifa.
Mnyama
Simba yeye ameamua kutuliza bunduki zake muhimu huko visiwani Zanzibar ambako
walienda jana.
Yanga
angalau wameambulia nafasi ya pili msimu huu baada ya kucheza mechi 25 na
kujikusanyia pointi 55 kibindoni,.
Simba
wao hali ni tete kwasababu wamepata nafasi ya nne kufuatia kushuka dimbani mara
25 na kujikusanyia pointi 37 katika nafasi ya nne, lakini kila timu ina mchezo
mmoja mkononi.
Abdallal
Kibadeni anayeifundisha Ashanti United kwasasa aliiongoza Simba katika mchezo
wa mzunguko wa kwanza na kufanikiwa kutoka sare ya 3-3 akianza kufungwa mabao
3-0 kipindi cha kwanza.
Kipindi
cha pili aliwatuliza vijana wake na kufanikiwa kusawazisha mabao yote matatu na kuleta shida
upande wa pili.
Baada
ya mechi hiyo, Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelu `Julio` walitimuliwa
kwa sababu ya timu kufanya vibaya mzunguko wa kwanza wakati ilianza kwa
kuongoza ligi.
Makocha
wa Simba na Yanga wanakuwa hatarini kupoteza kazi zao pindi timu hizi
zinapokaribia kukutana.
Kuna
idadi kubwa ya makocha waliotumiliwa kwa Simba kuifunga Yanga au Yanga kuifunga
Simba sc.
Kumbuka
Ernie Brandts aliwapa Yanga ubingwa, lakini sare ya 3-3 na kipigo cha desemba
21 mwaka jana katika mechi ya `Nani
Mtani Jembe` kiliotesha nyasi kibarua chake baada ya kufungwa mabao 3-1.
Brandts
alishutumiwa na uongozi wa Yanga na mashabiki kuwa ameshusha kiwango cha klabu
hiyo, lakini ukweli unabaki kuwa ni matokeo ya kipigo na sare aliyoyapa kutoka
Simba.
Viongozi
wa timu hizi mbili zenye uhasimu mkubwa huwa hawana masihara pale kocha
waliyemwajiri anashindwa kumfunga mtani.
Ukiwa
kocha wa Yanga unaweza kuwa mikono salama ukifungwa na Mgambo au Azam fc,
lakini kufungwa na Simba sc ni hatari sana, hata kwa upande wa Simba ni hivyo hivyo.
Kibadeni
alitimuliwa na mikoba yake kuchukuliwa na Mcroatia Dravko Logarusic, huku
kiungo wa zamani na nahodha wa Simba, Suleiman Abdallah Matola, `Veron`
akirithi nafasi ya kocha msaidizi iliyokuwa chini ya Julio.
Logarusic
ana ajira ya miezi sita katika klabu yake na hatima ya kibarua chake bila shaka
imebakia katika mechi ya jumamosi.
Kocha
huyu hajawahi kuonja machungu ya kufungwa na Yanga kwasababu tangu aanze kazi
aliwafunga Yanga katika mechi ya `Nani Mtani Jembe`.
Sasa
anaiongoza Simba iliyowajeruhi mashabiki wake kwa matokeo mabaya msimu huu
dhidi ya Yanga iliyokosa ubingwa.
Mechi
hii ni ya heshima kwa Simba sc na Yanga
kwasababu wote wamekosa ubingwa mbele ya Azam fc.
Mtihani
huu ni mkubwa mno kwa Logarusic , japokuwa yeye anasema hana presha kabisa
kwasababu ni mechi ya kulinda heshima tu kwake.
Loga
anasema anatambua mechi hii inazikitanisha klabu zenye historia kubwa nchini,
lakini hana shaka kabisa kwani ataweza kufanya vizuri.
Ukija kwa
upande wa Yanga, `Nani Mtani Jembe` ilimkosesha kibarua Mholanzi, Ernie Brandts
na msaidizi wake, Fredy Minziro na kazi zao kuchukuliwa na Mholanzi mwenzie,
Hans Van Der Pluijm na Mtanzania Charles Mkwasa.
Pluijm
hajawahi kukutana na presha ya mechi ya watani wa jadi, lakini viongozi wa
klabu wamemueleza umuhimu wa mechi hiyo.
Pluijm
anasema anajiandaa kufanya vizuri dhidi ya Logarusic anayeonekana kuichukuliwa
kirahisi mechi hiyo.
Pluijm naye
ana ajira ya miezi sita kama ilivyo kwa Loga na tayari ameshawakosesha ubingwa
Yanga.
Kilichobaki
kwake ni kulinda heshima ya klabu kwa kuwafunga Simba jumamosi.
Mkwasa
anaujua utamaduni wa klabu hizi mbili na lazima amemshauri Pluijm kuweka
mikakati mizito kwasababu kufungwa inaweza kuleta matatizo katika kazi yake.
Plujm arejee
nyuma ili kufahamu mambo yalivyokuwa mechi
ya mzunguko wa kwanza ambayo mwenzake alitoka
sare ya 3-3 na Yanga kufungwa 3-1 `Nani Mtani Jembe` .
Baada
ya matokeo hayo, atagundua kuwa Yanga wanahitaji kujipunguzia machungu ya
kukosa ubingwa kwa kuwafunga Simba sc, kwa maana hiyo ili kukwepa yaliyomkuta
Brandts lazima ajipange vizuri.
Loga na Pluijm watakutana
kwa mara ya kwanza katika mchezo huo hapa nchini na atakayeshinda atakuwa na
uhakika wa ajira ya mkataba mpya.
Loga alipoteza mchezo wa
mwisho dhidi ya Pluijm walipokuwa Ghana ambako Loga alikuwa akiifundisha Hearts
Of Oak, huku Pluijm akiwa na Berekum Chelsea ambapo Pluijm alishinda mabao 4-2.
Je, kati ya Logarusic na Pluijm nani kupata mkataba mpya jumamosi?
Hili ni swali
litakalojibiwa baada ya dakika 90 za mchezo wa watani wa jadi ndani ya dimba la
Taifa jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment