Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Balozi wa Canada nchini Mh.Alexandre Leveque na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo akimvika Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Bwana Ndesanjo alisema klabu hiyo imeamua kumtunuku Rais Kikwete medali hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini katika Nyanja mbalimbali kutokana na uongozi wake mahiri.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya Lions waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo kushiriki hafla ya kumtunuku Rais Kikwete medali maalumu ya Uongozi Bora na Mahusiano mema.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa SAGCOT Fund Balozi Ami Mpungwe baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salam leo(picha na Freddy Maro)
Home
»
»Unlabelled
» LIONS CLUB YAMTUNUKU RAIS KIKWETE MEDALI YA UONGOZI BORA
Friday, April 11, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment