NGWE ya mwisho ya uuzaji wa tiketi kuelekea kombe
la dunia litakalofanyika mwezi juni mwaka huu nchini Brazil imezinduliwa jana na
tiketi 126, 837 kati ya 199, 519 zilizotolewa na FIFA kwa mechi 54 kati ya mechi 64 ziliuzwa
ndani ya saa nne tu.
FIFA walisema wenyeji Brazil waliomba theluthi 2 katika
oda ya mwisho ambazo ni tiketi 80, 496, huku tiketi 46, 341 zikienda mataifa
mengine.
FIFA waliongeza kuwa vituo 12 vya kuuza tiketi
katika nchi mwenyeji vitafunguliwa Ijumaa , lakini maeneo ya Brasilia na Porto Alegre tiketi zitapatikana
kuanzia mwezi ujao tu.
Hata hivyo FIFA wamewaeleza mashabiki walionunua
tiketi kuwa wanatakiwa kupanga ahadi ya kuzikusanya kupitia mtandao wa
Fifa.com.
Kuanzia juni mosi hadi siku ya fainali Julai 13,
FIFA wamesema tiketi zitakuwa zikiuzwa kwenye vituo maalum nchini Brazil.
Mechi zilizouza zaidi tiketi katika ngwe hii ya
mwisho ni fainali ya Julai 13, juni 12 kati ya mwenyeji Brazil v Croatia,
Mexico v Cameroon, England v Italia, Argentina v Bosnia, Brazil v Mexico,
mabingwa watetezi Hispania v Chile, Cameroon vs Brazil, Croatia v Mexico na
Australia v Spain.
“Tumebakiwa na takribani miezi miwili kufikia
fainali za kombe la dunia, hii ni nafasi ya mwisho kwa mashabiki kujipatia
tiketi za michuano hii mikubwa zaidi duniani”. Alisema Thierry Weil ambaye ni
meneja mauzo wa tiketi wa FIFA.
Kufikia jana FIFA walisema jumla ya tiketi 2 577 662
tayari zilishauzwa.
0 comments:
Post a Comment