JURGEN Klopp amesema ana `sababu 1,000` za
kuendelea kubaki Borussia Dortmund na kukataa kujiunga na Manchester United.
Klopp amekuwa akihusishwa kuhamia Old Trafford
tangu David Moyes atimuliwe jumatatu ya wiki hii, lakini kocha huyo amekanusha
tetesi hizo.
Pia kocha huyo ameongeza kuwa hana mawasiliano yoyote
na viongozi wa juu wa Man United.
“Ni jambo baya kumkataa mtu kabla hajatuma ombi,
lakini haiwezekani” Klopp amewaambia waandishi wa habari.
Klopp aliyewahi kuifundisha Mainz kabala ya
kujiunga na Dortmund mwaka 2008, alisaini mkataba mpya mwezi oktoba mwaka jana
ambao utamfanya akae Signal Iduna Park hadi mwaka 2018.
Kocha huyo, 46, amekiri kuwa klabu ya Man United
ni kubwa, lakini hana mpango wa kwenda.
“Kuna sababu zaidi ya 1,000 za mimi kuwa na furaha
zaidi na klabu yangu”. Alisema Klopp.
Dortmund wanakabiliana na Bayer Leverkusen leo
katika uwanja wa Bay Arena, mechi ya
ligi kuu nchini Ujerumani, Bundesliga, huku wakiwa nafasi ya pili na wapo nyuma
kwa pointi 17 dhidi ya mabingwa Bayern Munich.
0 comments:
Post a Comment