Rais Jakaya Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, juzi. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi. Picha na Ikulu
..................................................................
Mbeya. Rais Jakaya Kikwete amemteua Profesa Mark Mwandosya kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) wakati Profesa Joseph Msambichaka akiteuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.
Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa Machi mwaka huu, Rais pia amemteua Profesa Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa taaluma, utafiti na ushauri, wakati Profesa Emmanuel Luoga ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa chuo atakayeshughulikia utawala, fedha na mipango.
Taarifa iliyotolewa jana na chuo hicho ilisema kuteuliwa kwa viongozi hao kunalenga kukiimarisha zaidi chuo ambacho kilipanda hadhi ya kuwa chuo kikuu tangu mwaka 2012.
Wakati huo huo, Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .
0 comments:
Post a Comment