Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo jijini Mbeya............................................................................................
WACHEZAJI 16 kati ya 34 wa
kikosi cha Maboresho ya Timu ya Taifa (Taifa stars) wamechaguliwa kutoka kwenye
kambi iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya
Rungwe mkoani Mbeya .
Kikosi hicho kimetangazwa leo jijini Mbeya na Kocha
Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa
Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo mjini humo.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mlinda mlango Benedict
Tinoko Mlekwa kutoka Mara.
Walinzi wa kati: Emma
Namwondo Simwanda kutoka Temeke na Joram Nason Mgeveja kutoka Iringa.
Walinzi pembeni : Omari
Ally Kindamba kutoka Temeke, Edward Peter Mayunga kutoka Kaskazini Pemba na
Shirazy Abdallah Sozigwa kutoka Ilala,viongo wa Ulinzi ni Yusufu Suleiman
Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi.
Viongo Washambuliaji: Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja
na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, na Viungo wa pembeni ni Omari
Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara.
Washambuliaji: Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu
Kassim Lipati kutoka Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na
Paul Michael Bundara kutoka Ilala.
Madadi aliongeza kuwa katika kikosi hicho pia wamechaguliwa
wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya wenye umri chini ya Miaka 20
ambao ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Atanas Fabian kutoka Mbeya.
Aidha Kocha huyo alisema wachezaji wengine walioachwa
wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa
sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.
Alisema Kambi ya timu hiyo ilianza Machi 22, Mwaka huu na
kuhitimishwa Aprili 17, mwaka huu kwa awamu ya kwanza ambapo wachezaji hao
watajiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maezo ya mechi ya
Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya
Pili.
0 comments:
Post a Comment