
RASMI
Abdallah Kibadeni `King Mputa` ameishusha daraja Ashanti United baada
ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa maafande wa Tanzania Prisons
`Wajelajela` katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania bara
uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Kibadeni
alikuwa anahitaji ushindi ili kubakia ligi kuu na hata kama angepata
sare angeshuka daraja na Ashhanti yake, lakini kipigo hicho kimemzika na
kuungana na JKT Oljoro na Rhino Rangers kushuka daraja.
Nao mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bar, Azam fc wameshinda bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu na kukabidhiwa kombe lake.
Bao la ushindi kwa Azam fc limefungwa na John Bocco `Adebayor`.
Azam fc wamefanikiwa kutwaa ubingwa wao wa kwanza msimu huu bila kupoteza mechi yoyote.
Yanga na Simba zimetoka sare ya bao 1-1 ndani ya uwanja wa Taifa.
Katika mechi nyingine Mbeya City fc wameshinda bao 1-0 dhidi ya Mgambo JKT katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
CoastalUnion wamelala bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Huko Arusha JKT Oljoro wamelazimisha sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, lakini wameshashuka daraja.
Nao maafande wa Rhino Rangers wamekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Ruvu Shooting katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
0 comments:
Post a Comment