
Na Baraka Mpenja, Dar Es Salaam
ABDALLAH Kibadeni au David Mwamwaja, lazima mmoja aishushe daraja timu yake katika dimba la Jamhuri Mkoani Morogoro.
Maaafande
wa jeshi la Magereza, Tanzania Prisons `Wajelajela` kesho wanahitimisha
ligi kuu soka Tanzania bara kwa kukabiliana na wauza mitumba wa Ilala,
Ashanti United uwanja wa Jamhuri.
Hii ni mechi ngumu mno na inahitaji maarifa makubwa kwa kocha wa Ashanti, Mzee Kibadeni na Mwamwaja wa Tanzania Prisons.
Kati ya timu hizi mbili, moja lazima iungane kushuka daraja na timu za JKT Oljoro ya Arusha na Rhino Rangers ya Tabora.
Timu zote zimecheza mechi 25 na kujikusanyia pointi 25. Kinachozitofautisha ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Prisons wamecheza mechi 25 ambapo wameshinda mechi 5, sare 10 na kupoteza mechi 10.
Wajelajela hao wamefumania nyavu mara 25 na kufungwa mabao 33. Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa unapata hasi (-8).
Ashanti United wameshinda mechi 6, sare 7 na kufungwa mechi 12.
Wamefunga mabao 20 na kufungwa mabao 38. Ukitoa mabao ya kufunga na kufungwa anapata hasi kumi na nane (-18).
Kwa wastani huo wa mabao ya kufunga na kufungwa, Prisons wanakuwa juu ya Ashanti United.
Katika msimamo, Prisons wapo nafasi ya 11, huku nafasi ya 12 ikikaliwa na Ashanti United, lakini zimefungana pointi.
Kuelekea
katika mechi hiyo, klabu zote zinahitaji ushindi, lakini Ashanti ndio
wahitaji wakubwa zaidi kwasababu wamezidiwa mabao mengi ya kufunga na
Prisons.
Endapo
Ashanti United watashinda mechi hiyo watafikisha pointi 28 na kuvuka
mkasi wa kushuka daraja, wakati Prisons watakuwa wameshashuka daraja.
Matokeo ya sare ya aina yoyote ile yatawashusha daraja Ashanti kwasababu ya wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Kama Prisons watapata sare siku hap kesho, watakuwa wamenusurika kushika daraja kwa faida ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Kocha
kibadeni alishasema kuwa hana cha kupoteza zaidi ya kushinda mechi
mbili za mwisho kuanzia ya jana dhidi ya Simba sc ambayo alipata matokeo
mazuri.
Sasa amebakiwa na mechi moja na Prisons, na inawezekana mikakati yake ni mkubwa mno kuhakikisha anashinda.
Naye
kocha mkuu wa Prisons, David Mwamwaja aliikuta timu ikiwa hoi chini ya
kocha Jumanne Chale ambaye ameishusha daraja Rhino Rangers.
Lengo
la Prisons kumfukuza Chale ilikuwa kutafuta kocha atayeinuru kushuka
daraja na ndipo walifanya uchaguzi sahihi wa kumpa mikoba Mwamwaja.
Chini ya Mwamwaja, Prisons imefanya vizuri na kufikia hapo ilipo.
Malengo ya Mwamwaja hayajatimia kama kwa Kibadeni, kwani wote walipewa timu ili wazinusuru kushuka daraja.
Kitendawili cha timu gani inashuka baina ya Prisons na Ashanti United kitageguliwa kesho uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment