MENEJA
wa Liverpool, Brendan Rodgers baada ya ushindi wa leo wa mabao 3-2
dhidi ya Nowrich amemsifia mshambuliaji wake kinda, Raheem Sterling na
kusema ndiye mchezaji bora zaidi kijana barani Ulaya.
Sterling
amefunga mabao mawili leo kati ya matatu na kuifanya Liverpool ishinde
mechi 11 mfufulizo na kuukaribia ubingwa baada ya miaka 24 kupita bila
taji.
Pia alitoa pasi kwa Luis Suarez na kumfanya afunge bao lake la 30 msimu huu.
“Nadhani
ni mchezaji bora zaidi kijana kwa mpira wa Ulaya, kwa upande wangu,
nadhani ingekuwa chini ya miaka 21. Kiukweli nimefurahishwa na kuimarika
kwake. Anatumia muda wake mwingi katika kazi yake”.
“Tumejitahidi kumchezesha nafasi tofauti ili kuongeza uwezo wake. Ni mtoto mwenye akili sana”.
Liverpool
wameongezwa morali baada ya kipigo cha jana cha Chelsea na sasa
wanahitaji pointi saba tu katika mechi tatu zilizosalia dhidi ya
Chelsea, Crystal Palace na Newcastle.
Akizungumzia
changamoto ya ubingwa, Rodgers alisema: “ Ninapenda ushindani ulivyo
mkubwa. Nimefanya kazi kwa muda mrefu nikiwa kocha kijana”.
“
Tangu nimeingia katika kazi hii nina miaka 15. Malengo yangu kama kocha
ni kuwaweka wachezaji kuwa bora zaidi na matokeo yake ni kushinda”.
“Kuishi
Liverpool ni faraja na heshima kwangu. Najua wachezaji wananipatia
ninachotaka, nimeshinda mechi 11 mfululizo, haya ni mafanikio kwangu”.
Amesema Rodgers.
0 comments:
Post a Comment