Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WAKATA miwa wa Kaitaba,
`Wanankulukumbi` Kagera Sugar wanatarajia kufanya usajili makini ili kuendana
na kasi ya ushindani katika mitanange ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu
ujao.
Murage Kabange, kocha msaidizi wa
Kagera Sugar amebainisha mapungufu kadhaa katika kikosi chao na sasa wapo
katika mipango ya kufanyia marekebisho.
“Kwanza majeruhi ya kudumu kwa baadhi
ya wachezaji wa kikosi cha kwanza ni tatizo lilituathiri sana”.
“Pili ubutu wa safu ya ushambuliaji
lilikuwa tatizo la kudumu kwa Kagera Sugar mpaka tunapozungumza hivi”.
“Tatu hatukuwa na wachezaji mbadala,
kwahiyo kila inapotokea mchezaji muhimu anapata majeruhi, ilikuwa janga kwetu”.
Kutokana na matatizo hayo, Kabange
alisema wanatarajia kuongeza nguvu sehemu ya ushambuliaji ambapo wanafikiria
kutafuta hata mchezaji wa kigeni.
“Tunadhani ipo haya ya kwenda hata nje
ya nchi ili kupata washambuliaji watakaotuongezea nguvu msimu ujao”.
“Lakini tunafirikia kutafuta wachezaji
wengi ili tuwe na machaguo mengi zaidi. Tutasajili vijana zaidi ili iwe rahisi
kufundishika”. Alisema Kabange.
Kagera Sugar waliomaliza msimu uliopita
katika nafasi ya tano kwa pointi 38 walikuwa wanamtegemea mshambuliaji wao nyota,
Them Felix `Mnyama` ambaye hata hivyo hakuonesha makali sana.
Pia Kabange alieleza kuwa wanafikiria
kuboresha safu yao ya ulinzi na kiungo.
Kagera Sugar walifungwa mabao 20 katika
mechi 26, huku wakifunga mabao 23.
Kwasababu hiyo, Kabange alisema kuna haja
ya kupunguza mabao ya kufungwa msimu ujao kwa kutafuta wachezaji watakaoongeza
nguvu katika ngome yao ya ulinzi.
Hata hivyo, Kabange alisema mabao 23 ya
kufunga katika mechi 26 yanadhihirisha ubutu wa safu ya ushambuliaji na kwa
kushirikiana na kocha mkuu, Mganda Jackson Mayanja wameona kuna haja ya
kutafuta washambuliaji wakali.
Aidha,
aliongeza kuwa msimu ujao wanatarajia kuingia katika mbio za ubingwa au nafasi
tatu za juu.
0 comments:
Post a Comment