Mgambo aliyetaka kumtwisha Nyundo mtoto Anna Yohana, akimbeba mtoto akiwa na hofu kuwa amemdhuru vibaya....
Baada ya
kujinasua na kupigana na mgambo zaidi ya saba, nikipiga simu kwa baadhi
ya waandishi wa habari huku Tape recorder ikiwa imeporwa.
*Ni kichanga cha miezi minne kilichofunikwa kwenye salfeti sokoni.
*Wauza magazeti nao wahaha meza zao kuvunjwa usiku wa manane.
NaChristopher Nyenyembe, Mbeya
MWANDISHI wa
Habari wa Gazeti hili (Tanzania Daima) mkoa wa Mbeya, Gordon Kalulunga,
ameambulia kipigo kutoka kwa mgambo wa jiji alipokuwa kazini akipiga
picha kwenye ‘operesheni vunja vunja’ sehemu ambayo mtoto mchanga wa
miezi minne alikuwa amelazwa na mama yake mzazi kwenye salfeti sokoni eneo la Kabwe Mwanjelwa.
Tukio hilo
lilitokea wakati wa sherehe za pasaka(jumatatu ya pasaka) baada ya
uongozi wa jiji la Mbeya kwa kutumia mgambo wake walipoamua kuendesha
operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara waliopanga bidhaa zao kando
kando ya barabara kuu ya Tanzania- Zambia katika eneo maarufu la
Mwanjelwa.
Mwandishi
Kalulunga alikutwa na mkasa wa kupigwa na mgambo zaidi ya saba na
kusababisha purukshani kubwa mara alipofanikiwa kupiga picha
zilizowahusu mgambo hao waliokuwa wakivunja vibanda na kuwatimua
wafanyabiashara ndogo ndogo waliopigwa marufuku kupanga bidhaa zao
kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa lengo la kuweka usafi wa jiji hilo.
“Nilikuwa natimiza wajibu wangu wa kazi kama mwandishi wa habari,alitokea mwanamke mmoja
aliyekuwa amevaa gauni refu la rangi ya njano na kunikaba shati,ndipo
mgambo wa jiji walipokuja na kuanza kunipiga,ilibidi kamera yangu
nimkabidhi polisi mmoja lakini nimepoteza redio yangu ya
kurekodia”alisema Kalulunga.
Alisema
baada ya tukio hilo kutokea ilibidi akatoe taarifa kwenye kituo kidogo
cha polisi Mwanjelwa na kupewa fomu ya kwenda kutibiwa (PF 3) ambako
ilibidi apatiwe matibabu na aliporudi polisi Mwanjelwa alitakiwa na mkuu
wa kituo hicho akatoe maelezo yake kituo kikuu cha polisi mjini kwa OC
–CID au mkuu wa polisi wilaya (OCD).
Kitendo cha
Mwandishi huyo kushambuliwa akiwa kazini kulisababisha habari za haraka
zisagae jijini humo na kisha kumfikia Kamanda wa Polisi mkoa huo,Ahmed
Msangi aliyeongea moja kwa moja na Kalulunga ili aweze kufahamu aina ya
uvunjifu wa amani uliojitokeza wakati wa operesheni vunja vunja
iliyokuwa akifanywa na mgambo hao ambao imechangia pia kuvunjwa vibanda
vya kuuzia magazeti tangu zoezi hilo lilipoanza.
“Namshukuru
sana mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya,Richard Mchomvu ametumia busara
kubwa sana kunikutanisha na kiongozi wa operesheni hiyo kutoka idara ya
afya aliyejulikana kwa jina la Odas na mkuu wa mgambo pamoja na bosi
wangu kazini,jiji wamekiri kunifanyia kitendo hicho eti walikuwa
hawafahamu kama mimi ni mwandishi” alisema Kalulunga.
Kufuatia
tukio hilo lililotulizwa na Mchomvu aliushauri uongozi wa jiji hilo
kushirikiana na vyombo vya habari katika majukumu yake kwa kuwa wananchi
wanapaswa kuelimishwa zaidi kila jambo linapofanyika na kusisitiza kuwa
usafi wa jiji ni muhimu hivyo kila upande una jukumu lake hivyo hawana
sababu yoyote ya kuonyeshana ubabe.
“Nikiwa mkuu
wa polisi wa wilaya sipendi kuona haki za binadamu zikivunjwa
kienyeji,uhai wa kila mtu ni muhimu zaidi,tumieni vyombo vya usalama
kuweka mambo yenu vizuri,waandishi nao wana jukumu kubwa la kuwasaidieni
watumieni,angalieni sasa mmepoteza kifaa chake cha kazi,naomba suala
hili mlimalize kwa ustaarabu hata Mkurugenzi anapaswa kujua” alisema
Mchomvu.
Kufuatia
tukio hilo na mtoto mchanga aliyenusurika kupigwa nyundo wakati mgambo
hao wakiendelea kubomoa vibanda,operesheni hiyo ilisitishwa mara moja
katika eneo hilo baada ya mama mzazi wa mtoto huyo alipofanikiwa kutimua
mbio na kumuacha mwanae aliyeangukia kwenye mikono ya wasamaria.
Wakati hali hiyo ikitokea,wauzaji wa magazeti jijini humo wamelalamikia zoezi hilo ambalo limewasababishia hasara
kubwa baada ya meza zao kuvunjwa usiku wa manane wakati uongozi wa jiji
hilo unafahamu fika aina ya meza zilizoruhusiwa kuwepo kwa ajili ya
kuuzia magazeti na haijulikani mahali zilipotupwa.
Jiji la Mbeya limekubali kulipa kifaa kilichoibwa/kupotea katika tafra
0 comments:
Post a Comment