Manchester United wanaweza kuwa wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa kireno William Carvalho.
Mchezaji huyo wa Sporting Lisbon William Carvalho amekuwa kwenye rada
ya David Moyes msimu huu huku akiwatuma maskauti kwenda kumuangalia
kiungo huyo mwenye miaka 22.
Ripoti kutoka Ureno sasa zinasema kwamba United wameshatuma ofa ya
£35m ili kumsajili kiungo huyo mkabaji ambaye pia ameivutia klabu ya
Real Madrid.
United bado hajawajathibitisha dili hilo kama limekamilika lakini
Carvalho ni mtu sahihi ambaye wanamhitaji katika kuijenga upya klabu yao
hasa katika eneo la kiungo ambalo limekuwa tatizo kuu la timu hiyo.
Mashetani wekundu na Sporting Lisbon wamekuwa na uhusiano mzuri wa
kibiashara – Cristiano Ronaldo na Nani walitoka Sporting kwenda United.
Pia Luis Nani anaweza kuhusishwa kwenye dili hilo.
0 comments:
Post a Comment