KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe
Scolari anaamini Atletico Madrid itaitupa nje Chelsea katika michuano ya UEFA
msimu huu.
Chelsea ilitoa suluhu ya bila kufungana na
Ateletico katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali katika dimba la Vicente
Calderon jumanne ya wiki hii, na kumuweka Jose Mourinho katika nafasi ya
kufanya vizuri wiki ijayo dimba la Stamford Bridge.
Hata hivyo, Scolari amesema Chelsea itatolewa,
huku sababu zake zikiwa za ubinafsi zaidi.
Kocha huyo anaiombea mabaya Chelsea isifuzu fainali mei 24 mwaka huu ili wachezaji
wake tegemeo David Luiz, Oscar, Willian na Ramires wapate muda wa kupumzika
“Kwetu itakuwa vizuri kwa Atletico kuwatoa
Chelsea, kwasababu itawapa wachezaji wangu wanne fursa ya kupumzika”. Scolari
amewaambiwa waandishi wa habari.
Scolari amethibitisha kuwa beki wa Chelsea, Luiz atakuwa
moja ya wachezaji wa kikosi cha kwanza katika michuano ya kombe la dunia majira
ya kiangazi mwaka huu nchini kwao Brazil.
“Wachezaji niliowachagua kuwa viongozi ni David
Luiz, Julio César na Fred," .
“Nimeshawachagua tayari na nimekuwa nikizungumza
nao mara kwa mara”
“Sina wasiwasi na orodha ya mwisho ya kikosi changu,
lakini nitasubiri ligi ziishe”.
Scolari amesisitiza kuwa hana wasiwasi juu ya
Neymar ambaye ni majeruhi kwasasa kwasababu anaamini atakuwepo katika fainali
za mwaka huu licha ya kutokuwa na msimu mzuri FC Barcelona.
“Neymar atakaribishwa vizuri timu yake ya taifa. Sijali
ukosoaji wa Kihispania juu ya mchezaji huyu”.
“Tunajua klabu yake haina mafanikio kwa sasa,
lakini Brazil ina aina yake ya uchezaji wa mpira, hivyo Neymar atakuwepo”.
0 comments:
Post a Comment