Majirani wakimuhudumia majeruhi
.............................................................................
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la London Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata
ya Mbebe Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake
na watu watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku
April 19 mwaka huu baada ya mmoja kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee
huyo kisha kubisha mlango akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea
njia.
Mzee London alipotoka nje ya nyumba akiwa
anamwelekeza njia mtu huyo anayedaiwa kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka
nyumbani kwake alifunikwa na kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na
kukatwa nyeti zake ambazo waliondoka nazo.
Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga
amesema baada ya unyama huo Mzee London alipoteza fahamu na alipozinduka
alipiga yowe kuomba msaada ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa
kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio
hilo.
Kwa mujibu wa Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa
watuhumiwa wa tukio hilo wanatokea Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa
na mhanga wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa
Hospitali ya Rufaa Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa
11:00 jioni April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya
Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha
awali imedaiwa sababu za kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu
aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa
mdogo wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa
na wengine kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani
imedaiwa watuhumiwa kuimbilia nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho
cha kikatili.
Kamanda Msangi ametoa wito kwa jamii kuacha tabia
za kujichukulia sheria mkononi amesema pindi wanapokuwa na migogoro ni vema
kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika
na tukio hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna
mtu aliye juu ya sheria.
NA Ezekiel Kamanga,Ileje Mbeya.
Mbeya yetu
|
0 comments:
Post a Comment