BAADA
ya kulaumiwa kuwa kiwango cha Bayern Munich kimeshuka kwa siku za karibuni,
kocha mkuu Pep Gaurdiola anaamini timu yake itarudi katika kiwango chake dhidi
ya Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Guardiola
amewasifu vijana wake kwa kuonesha kiwango kizuri katika mazoezi, na kusema
kuwa watarudisha makali yao ya msimu uliopita katika michuano hiyo mikubwa kwa
ngazi ya klabu.
Kikosi
cha Bayern tayari kimeshafanikiwa kutwaa ubingwa wa Bundesliga na sasa kinaliwinda
kombe la UEFA na DFB-Pokal.
Wakitokea
katika mafanikio ya kuwatoa Manchester United robo fainali ya UEFA, Bayern walikula
kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa ligi dhidi ya Borussia Dortmund jumamosi iliyopita .
Pia
wakitokea katika mafanikio ya kufuzu fainali ya DFB-Pokal kwa ushindi wa mabao
5-1 dhidi ya Kaiserslautern katikati ya wiki, Bayern watawavaa Eintracht
Braunschweig katika mchezo wa ligi kabla ya
kukabiliana na Real Madrid wiki ijayo.
Guardiola
amekubali kufanya makosa mechi chache zilizopita na ndio maana wachezaji wake
wamekuwa wakijituma zaidi katika mazoezi ili kurudi reline.
“Mechi
dhidi ya Braunschweig ni muhimu sana kwetu. Ni kipimo kizuri kabla ya kucheza
na Real Madrid”.
“Nina
uhakika mbele ya Real Madrid moja ya klabu bora zaidi duniani, tutajipanga
vizuri na kuonesha kiwango cha juu”.
‘Baada
ya kichapo cha Borrusia tumeboresha zaidi mazoezi, Matokeo yale yalikuwa makosa
yangu na sio wachezaji”. Alisema Guardiola.
Guardiola
ataingia katika mchezo wa wikiendi wa Bundesliga bila mlinda mlango wake namba
moja Manuel Neuer na beki David Alaba ambao ni majeruhi.
Alaba
anaumwa, laki I taarifa nzuri kwa Guardiola ni kuwa Thiago Alcantara
aliyekuwepo nje ya uwanja kwa wiki nane kwa majeruhi ya goti, sasa anaendelea
vizuri na anaweza kucheza.
0 comments:
Post a Comment