RYAN Giggs ameanza vizuri
kazi yake akiwa meneja wa muda wa Manchester United baada ya kuilaza Nowrich
City mabao 4-0 katika mechi ya ligi kuu soka nchini England kwenye uwanja wa
Old Trafford.
Wayne
Mark Rooney amefunga mabao mawili, huku Juan Mata aliyeanzia benchi leo hii naye
akifunga mabao mawili.
Giggs
ambaye kwa muda mrefu ameitumikia klabu ya Man United akiwa mchezaji,
aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda baada ya David Moyes kufukuzwa kazi jumanne
ya wiki hii.
Matokea
ya leo ni mabaya mno kwa Nowrich City kwasababu yanawaweka katika hatari ya
kushuka daraja, huku wakibakiwa na mechi ngumu dhidi ya Asernal na Chelsea.
Baada
ya mechi ya leo, Nowrich wanabakia katika nafasi ya 17 kwa pointi zao 32
kufuatia kushuka dimbani mara 36.
Man
United wanabakia nafasi yao ya 7 kwa kujikusanyia pointi 60 baada ya kucheza
mechi 35.
Rooney
baada ya kuchangia ushindi wa leo amesema kuwa anaamini Giggs ana kila sifa ya
kuwa meneja wa kudumu wa Manchester United.
“Ilikuwa
tofauti kabisa leo chini ya Giggs”. Rooney ameuambia mtandao wa Sky Sports.
“Nimecheza
naye kwa miaka 10, lakini wote tunajua kuwa ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa na
amekuwa sehemu ya benchi la ufundi msimu uliopita”.
“Anajijenga
kuwa kocha. Sisi kama timu tunaona hilo”
“
Tunaona jinsi alivyoanza majukumu yake baada ya kuteuliwa”
“
Imekuwa furaha kupata ushindi mbele yake”. Amesema Rooney muda mfupi baada ya
mechi kumalizika.
Rooney
ameongeza kuwa kila kitu kipo chini ya bodi kwasababu wao ndio wenye mamlaka ya
kuchagua nani kuwa kocha mkuu na hakuna anayejua, lakini Giggs anastahili
kushika nafasi hiyo.
Mata
kwa upande wake baada ya kutokea benchi na kufunga mabao mawili amesema ana
furaha ya kufanya kazi chini ya Giggs.
“Kwa
upande wangu ninajisikia furaha kufanya kazi chini yake”.
“Tangu
nikiwa mdogo, nakumbuka alikuwa anacheza.”
“
Ni mtu mzuri wa Man United. Unaweza kusema alizaliwa hapa na nadhani wachezaji
wote wanajisikia vizuri kuwa naye katika mazoezi”.
“Lakini
lipo juu ya uwezo wetu, maamuzi ni juu ya bodi. Acha tufurahi tukiwa naye mpaka
mwisho wa msimu”. Alisema Mata.
MATOKEO YA MECHI ZOTE HAYA HAPA CHINI
ENGLAND: Premier League | |||||||
14:45 | Finished | Southampton | 2 - 0 | Everton | |||
17:00 | Finished | Fulham | 2 - 2 | Hull City | |||
17:00 | Finished | Stoke City | 0 - 1 | Tottenham | |||
17:00 | Finished | Swansea | 4 - 1 | Aston Villa | |||
17:00 | Finished | West Brom | 1 - 0 | West Ham | |||
19:30 | Finished | Manchester United | 4 - 0 | Norwich |
0 comments:
Post a Comment