David
Moyes atalipwa fidia ya £5million baada ya kufukuzwa kazi na Manchester
United – ikiwa ni kipengele cha makubaliano ya mkataba wake na klabu
hiyo.
Kocha huyo wa zamani wa Everton amekaa miezi 10 tu katika
mkataba wake wa miaka 6 na, hatua hiyo imekuja baada ya kuwa na
mfululizo mbaya wa matokeo.
Katika mkataba wa Moyes na United kulikuwa na kipengele
kinachoeleza ikiwa Manchester United ingefeli kufuzu kucheza Champions
League msimu huu basi ikatokea United wakaamua kusitisha mkataba wake
basi fidia isingezidi mshahara wake wa miezi 12 ambao ni £5million.
0 comments:
Post a Comment