BILA
mchezaji bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo, Real Madrid wanaingia kata EL
CLASICO ya 3 na ya mwisho kwa Msimu huu dhidi ya FC Barcelona usiku wa leo
katika uwanja wa Estadio Mestalla Mjini Valencia.
Hii
ni fainali ya Fainali ya Kombe la Mfalme, Campeonato
de España – Copa de Su Majestad el Rey, kwa kwetu limezoeleka kwa
jina la Copa del Rey.
Barcelona,
ambao wameshatwaa Kombe hili mara 26, mara ya mwisho kulitwaa ni 2012, wakati
Real, ambao wamelitwaa mara 18, Mwaka Jana walifungwa katika mechi ya fainali
na mahasimu wao Atletico Madrid.
Barca
na Real zimeshakutana mara mbili Msimu huu kwenye mechi za ligi kuu maarufu
kama La Liga, huku Barca wakishinda
Mechi zote mbili.
Mara ya mwisho kukutana kwenye Copa del Rey ni
Mwaka 2011, tena Uwanja huu huu wa safari hii, Estadio Mestalla, ambapo Bao la
Dakika za Majeruhi la Cristiano Ronaldo liliwapa Kombe Real na pia kumpa Kombe
la Kwanza Kocha Jose Mourinho kwenye himaya yake na Real Madrid.
MECHI 3 ZILIZOPITA:
-Real
3 (Benzema 2, Ronaldo) Barcelona 4 (Iniesta, Messi 3), La Liga, Machi 2014
-Barcelona
2 (Neymar, Sanchez) Real 1 (Jese), La Liga, Oktoba 2013
-Real
2 (Benzema, Ramos) Barcelona 1 (Messi), La Liga, Machi 2013
Lakini
safari hii kila Klabu ina Meneja mpya, Carlo Ancelotti na Real na Gerardo
Martino kwa Barca, na wanatinga kwenye Fainali hii wakitokea kwenye matokeo
tofauti kabisa.
Barca
wanatinga Fainali hii wakiwa kwenye majonzi makubwa kwani Wiki moja iliyopita
walikuwa kwenye ndoto kubwa ya kutwaa Trebo kama walivyofanya Mwaka 2009 lakini
mambo yakapinduka na wakatolewa toka UEFA na Atletico Madrid na Siku 3 baadae
kufungwa 1-0 na Granada kwenye La Liga na kuachwa wakiwa Pointi 3 nyuma ya
Vinara Atletico na Real huku Mechi zikiwa zimebaki 5.
Tofauti
kabisa, Real wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na morali ya juu baada ya kufuzu
kuingia Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na pia kuwa kileleni mwa La Liga,
pamoja na Atletico, baada ya kuifumua Almeria 4-0 Siku 3 baadae.
Kila
Timu inakabiliwa na Majeruhi wengi huku Barca ikiwa dhoofu kwenye safu yao ya
ulinzi wakiwemo Gerard Pique, Carles Puyol na Marc Bartra, ambaye kidogo ni
nafuu na huenda akacheza, lakini upo uwezekano mkubwa kwenye Mechi hii Difensi
ya Barca ikawa na Viungo, Mascherano na Busquet, kama Masentahafu wao.
Real
wataingia wakiwa na hatihati kuhusu kucheza kwa Staa wao Cristiano Ronaldo
ambae hajacheza Mechi 2 zilizopita akiwa na maumivu.
Carlo
Ancelotti ameleeleza jana kuwa Ronaldo hatakuwepo, lakini kukosekana kwake
kunaweza kutoa mwanya kwa ama Asier Illarramendi au Isco kucheza na kuungana na
Angel di Maria, Gareth Bale na Karim Benzema kwenye mashambulizi.
Ancelotti
mapema jana alikaririwa akisema Ronaldo anaweza kucheza kwasababu anaendelea
vizuri, lakini baadaye kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi ya
leo alithibitisha kuwa nyota huyo atakosekana kabisa.
“Cristiano
Rinaldo hatakuwepo, lakini tuna wachezaji wengi katika kikosi chetu”.
“Tuna
imani kubwa na timu hii. Nimekuwa nikijitahidi kukabiliana na majeruhi na
nadhani tutafanya kazi nzuri tu”. Aliongeza kocha huyo raia wa Italia ambaye
hata hivyo aligoma kutaja kikosi kinachoweza kuanza leo hii.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Real Madrid: Casillas;
Carvajal, Ramos, Pepe, Coentrao; Modric, Alonso, Illarra; Di Maria, Benzema,
Bale
Barcelona: Pinto; Alves, Mascherano,
Bartra, Alba; Busquets, Xavi, Iniesta; Neymar, Messi, Sanchez
COPA del REY-NJIA YA FAINALI
NUSU FAINALI
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2]
Jumanne Februari 11
Atletico
de Madrid 0 Real Madrid
CF 2 [0-5]
Jumatano Februari 12
Real
Sociedad 1 FC Barcelona 1 [1-3]
FAINALI
Aprili 16
Real
Madrid v Barcelona
0 comments:
Post a Comment