Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
AFISA habari wa klabu ya Coastal Union, Hafidh
Kido ametangaza kubwaga manyanga kutokana na migogoro inayoendelea katika klabu
hiyo.
Akiongea na mtandao huu jioni ya leo, kido amesema
kitaaluma yeye ni mwandishi wa habari na hatakiwa kuwa upande wowote, hivyo
ameamua kujitoa katika nafasi yake.
“Kila nilichokuwa nakifanya Coastal ilikuwa ni
kujitolea na si kwa masilahi. Coastal ni klabu yangu na sikuwa na mkataba,
lakini nimefanya kazi zao bila tatizo kwasababu naipenda timu hii”. Alisema
Kido.
Kido aliongeza kuwa maamuzi yake ameyachukua bila
kushinikizwa na mtu yoyote.
Haya yamekuja siku chache baada ya aliyekuwa
mfadhili wa klabu hiyo, mkurugenzi Mkuu
wa kampuni ya Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum Bin Slum kuondolewa na uongozi wa klabu hiyo.
Bins Slum leo hii amesema ataendelea kuwepo
Coastal Union kwa kutoa msaada pale itakapobidi.
“Kama viongozi makini watakuwepo nitajitahidi
kuisaidia timu yangu kwasababu mimi ni mwanachama, lakini kwa uongozi wa sasa
siwezi kutoa kitu chochote”.
“Mimi sikuwa mdhamini, nilikuwa mfadhili kwa
maandeleao ya klabu. Viongozi wamesema maneno mabaya juu yangu, lakini ni
changamoto tu. Nitahakikisha nipo Coastal Union”.
Bin Slum amesema kwamba ametumia zaidi ya Sh.
Milioni 300 kwa ajili ya Coastal Union ya Tanga ndani ya kipindi cha miaka
minne, lakini ajabu malipo yake kukashifiwa.
0 comments:
Post a Comment