UVUMILIVU
umemshinda mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Javier Harnandez
`Chicharito` na sasa ameitaka klabu yake kumuuza majira ya kiangazi mwaka huu
baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.
Chicharito
ameongea mara tatu na bosi wake David Moyes katika miezi miwili iliyopita juu
ya yeye kunyimwa nafasi ya kucheza, huku akianzishwa katika mechi tano tu za
ligi kuu msimu huu.
Nyota
huyo raia wa Mexico ameiambia klabu yake kuwa atasikiliza ofa zikazokuja juu
yake majira ya joto na hadhani kama yupo katika mipango ya Moyes hapo baadaye.
Chicharito
ameshindwa kupata namba ya kudumu mbele ya Wayne Mark Rooney, Robin Van Persie
na Danny Welbeck.
Sasa
mshambuliaji huyo amefikia maamuzi ya kuondoka huku akihusishwa na mpango wa
kuhamia Atletico Madrid kama mrithi wa Diego Costa mwenye kila dalili ya
kujiunga na Chelsea majira ya kiangazi.
Chicharito
mwenye miaka 25 alihuzunishwa baada ya kukosa nafasi ya kuanza kwenye mechi ya robo fainali ya UEFA dhidi ya
Bayern Munich, huku kocha Moyes akimuanzisha Rooney ambaye hakuwa fiti kwa
mechi ile.
Siku
nne Kabla ya kuwakabili Bayern, Chicharito alicheza dakika 90 katika mechi ya
ligi kuu dhidi ya Newcastle ambapo walishinda 4-0, hivyo alijiona kuwa
anastahili kuanza katika kikosi cha Man United kwa kuzingatia kiwango chake
kwenye mechi ile na mazoezi ya kujiandaa
na safari ya Allianz Arena.
Msimu
huu, mshambuliaji huyu amecheza mechi 31 katika mashindano yote, na ameanzia
benchi kwenye mechi 20, huku akifunga mabao 9 katika msimu huu mgumu kwa David
Moyes.
Nahodha
wa Man United, Nemanja Vidic naye yuko mbioni kujiunga na Inter Milan, wakati
huo huo Rio Ferdinand, Patrice Evra, Shinji Kagawa, Nani, Anderson na Alex Buttner ni miongoni mwa wachezaji wengi
wanaotarajiwa kuondoka Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment