Robo fainali ya Champions league inaendelea leo baada ya Manchester United kutoka sare ya 1-1 na Bayern - wakati Barca nao walitoka sare ya 1-1 na Atletico. Leo hii Real Madrid wapo nyumbani wakiwakaribisha Dortmund na PSG wanaumana na Chelsea jijini Paris.
Real Madrid vs Borussia DortmunD
Kwa
upande wa Real Madrid, wishlist yao ilikuwa simple kidogo; Avoid Bayern
Munich and Barcelona! Na kama wangeruhusiwa kujichagulia timu, bila
shaka wangechagua Atletico Madrid au Manchester United.
Katika
draw hii Real wamepewa Borussia Dortmund. Hii unaweza kusema ni
repetition ya semi final ya mwaka jana ambapo Madrid waliambulia kichapo
cha mbwa mwizi na kutolewa kwenye mashindano kwa aggregate ya mabao
4-3. Katika ushindi huo, ambapo Robert Lewandoski alifanikiwa kufunga
mabao manne katika first leg, season hii amekuwa suspended kwenye first
leg itakayofanyika Bernabeu na hiyo ni boost kubwa kwa Real kufanya
revenge. Pia timu hizi mbili zime move katika directions mbili tofauti
katika kipindi hiki cha miezi 12, Real Madrid chini ya Carlo Ancelotti
imekuwa tishio zaidi na wapo katika nafasi nzuri ya kuchukua ubingwa wa
Spain, wakati Dortmund wao wanaonekana ku struggle katika ligi yao huku
wakiandamwa na majeruhi ya key players wengi waliocheza kwenye katika
nusu fainali iliyopita ya Jurgen Klopp kuwa ngumu kiasi dhidi ya Madrid
TAKWIMU
Real
Madrid wanafanikiwa kuingia kwenye robo fainali kwa msimu wa nne
mfululizo, na wameshinda kuvuka hatua ya nusu fainali kwenda fainali
katika misimu mitatu mfululizo.
Rekodi
ya Madrid ya nyumbani dhidi ya timu za Ujerumani ni Ushindi mechi 19,
sare 4 na kufungwa 2, mechi mbili hizo wamefungwa na Bayern mwaka 2000
na 2001, Bayern ndio pekee ya Ujerumani iliyofanikiwa kushinda Santiago
Bernabeu. Rekodi ya jumla ya Madrid dhidi ya timu za Ujerumani katika
UCL - W12 L8.
Rekodi
ya Dortmund dhidi ya timu za La Liga ni ushindi mechi 5 na wamefungwa
2, wameweza kushinda mara 1 tu katika ardhi ya Spain.
Msimu uliopita Madrid walitolewa na Dortmund nusu fainali , je msimu huu wataweza kuvuka kizingiti cha watoto wa Jurgen Klopp?
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Pande
zote mbili hazitakuwa too upset na draw hii. Kama ikikubalika kwamba
Real Madrid na Bayern Munich are the class of this year`s competition,
ukiacha Barca, PSG na Chelsea ndio next favourites kwenye mashindano.
PSG
na Chelsea wote wanaonekana impressive kwa namna tofauti, walifanikiwa
kufika hapo walipo baada ya kuwatoa Bayern Leverkusen na Galatasaray
kwenye round iliyopita.
Kivutio
kikubwa katika mechi za Chelsea mara nyingi kimekuwa maneno ya mbwembwe
kutoka kwa manager wake, Jose Mourinho (the special one) ambaye
anajivunia kikosi imara kinachoweza kuitikisa timu yeyote, mfano mzuri
waulize mashabiki wa Arsena!
Kwa
upande wa PSG wakiwa chini ya mchezaji wa zamani maarufu, mfaransa
Laurent Blanc wakiwa wanaundwa na kikosi chenye wachezaji matata kama,
Edison Cavan na thiago Mota Zlatan Ibrahimovich ambapo Chelsea kama
wanataka kufika hatua ya nusu fainali basi ni lazima waweke mikakati ya
kuwanyamazisha.
TAKWIMU
Mara
ya mwisho timu hizi zilipokutana katika hatua ya makundi ya michuano
hii msimu wa 2004/05, Chelsea walishinda 3-0 jijini Paris, goli la
kichwa la John Terry, na mengine mawili kutoka kwa Didier Drogba - na
kumpa Mourinho ushindi wa kwanza katika UCL akiwa na Chelsea baada ya
kutoka Porto.
Mara ya mwisho PSG kucheza nusu fainali ilikuwa msimu wa 1994/95 walipofungwa na AC Milan.
PSG
hawajafungwa kwenye uwanja wa nyumbani katika mechi 28 za ulaya. Timu
ya mwisho kushinda Parc des Princes katika michuano ya UEFA ilikuwa ni
Hapoel Tel-Aviv.
Chelsea wapo katika kuisaka nusu fainali ya 7 katika misimu 11 iliyopita - je wataweza kuwanyoosha Ibrahimovic na wenzie?
0 comments:
Post a Comment