KUNA
taarifa zimezagaa kuwa kocha wa Manchester United, David Moyes
amefukuzwa kazi, japokuwa haijathibitishwa na familia ya Glazer ambao
ndio wamiliki wa klabu hiyo.
Inasemekana
familia ya Glazer imefikia maamuzi ya kumfukuza kazi bosi huyo wa Man
United ikiwa ni miezi 11 tu tangu arithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Msemaji
wa Man United amegoma kueleza kama kweli Moyes amefukuzwa kazi,
lakini imefahamika kuwa kocha huyo hatakuwepo katika mchezo ujao dhidi
ya Nowrich City kwenye uwanja wa Old Trafford jumamosi .
Kocha
mchezaji Ryan Giggs anatarajiwa kuiongoza Man United mpaka mwishoni mwa
msimu, na wakati huo huo wasaidizi wa Moyes Steve Round, Phil Neville
na Jimmy Lumsden pia wanatarajiwa kuondoka na bosi wao.
Kocha wa kudumu wa Mashetani wekundu anatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa msimu huu.
Familia
ya Glazer amechukizwa na kipigo cha jana cha mabao 2-0 dhidi ya Everton
na kuwa mechi ya 11 kwa Man United kupoteza katika mashindano yote
mwaka huu.
Moyes
alisaini mkataba wa miaka 6 mwezi mei mwaka jana kurithi mikoba ya Sir
Ferguson aliyestaafu, lakini ameshindwa kupata mafaniko.
Baada
ya familia Glazer kufahamu kuwa Man United haitamaliza ligi katika
nafasi nne za juu, wameamua kuotesha nyasi kibarua cha Moyes.
Man
United wanaelekea kuwa mabingwa watetezi waliofanya vibaya zaidi katika
historia ya ligi kuu England kwa kuwa nafasi ya 7 na kwa mara mwisho
Ray Harford alifanya hivyo na Blackburn Rovers mwaka 1996. Pia
wanatarajia kukosa hata ligi ya Europa msimu ujao.
Bodi
ya ukurugenzi ya Man United imekuwa ikimvumilia Moyes kwa matokeo
mabaya, lakini walikerwa sana hasa walipofungwa nyumbani na wapinzani
wao wakubwa Liverpool na Manchester mwezi uliopita.
Imefahimika
hata wachezaji muhimu wa Man United wakiwemo , Robin van Persie,
Nemanja Vidic, Rio Ferdinand, Danny Welbeck, Javier Hernandez na Giggs, hawana furaha na Moyes.Mtandao huu unafuatilia `ngado kwa ngado` kujua hatima ya Moyes
0 comments:
Post a Comment