Friday, April 25, 2014

Muwezeshaji katika semina ya kuripoti habari za sanaa na utamaduni, Bwana Imani Mani alisema waandishi wa habari wana wajibu wa kukuza sanaa na utamaduni wa nchi.
Imani ambaye ni mwandishi mkongwe wa habari za sanaa na utamaduni katika Gazeti la serikali la `Daily News` alikuwa miongoni mwa wawezeshaji wa semina hiyo iliyofanyika shule kuu ya uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma (SJMC) kuanzia jana aprili 24 na kuhitimishwa leo aprili 25.
Malengo ya semina hiyo iliyodhaminiwa na SJMC kwa kushirikiana na shirika la GOETHE INSTITUT linalomilikiwa na wajerumani yalikuwa ni kuwafundisha wanafunzi wa  SJMC namna ya kuandika habari za sanaa na utamaduni kwa nia ya kuwaongezea maarifa zaidi.
Bwana Daniel (wa kwanza kulia) kutoka GOETHE, Bwana Abdallah Katunzi ( katikati) ambaye ni mwalimu wa SJMC  na Florence Muller  ( wa kwanza kushoto) kutoka GOETHE walikuwa waratibu wakuu wa semina hiyo.
 Waratibu wakuu wa semina na washiriki kwa pamoja walifurahia mada iliyowasilishwa na Imani Mani (hayupo pichani) na kujikuta wakiwa makini muda wote.
Mratibu wa semina ambaye ni mwalimu wa SJMC, Bwana Abdallah Katunzi (wa kwanza kulia) na muwezeshaji, Bw. Imani Mani (katikati) walizingatia muda huu muhimu kwa maisha ya binadamu. Waswahili wanasema `kazi na dawa`.
Christian Edward (wa kwanza kulia), Florence Muller (wa pili kulia), Annastazia Gura (wa tatu kulia), Victoria Mhagama ( wa nne kulia) na Carol Moshi (wa tano kulia) waliona ni muhimu kutunza matumbo yao kabla ya kurejea ukumbini kuendelea na semina.
Washiriki Annastazia Gura na Victoria Mhagama 
Mambo ya kuweka afya vizuri kabla ya kurejea kwenye semina
 Muwezeshaji wa semina, Bwana Imani Mani na Mkurugenzi wa GOETHE INSTITUT, Eleonore Sylla (kulia) wakimsikiliza mshiriki wa semina wakati akitoa mawazo yake (hayupo pichani)
Mratibu wa semina Bwana Abdallah Katunzi na Mkuu wa shule kuu ya Uandishi wa habari na mawasiliano kwa Umma (SJMC), Dkt. Herbert Makoye (kulia) wakiweka mambo sawa kabla ya zoezi la kugawa vyeti kwa washiriki kuanza
Mhariri mkuu wa Tovuti ya www.fullshangweblog.com, na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mpenja MEDIA company LTD inayomiliki blog ya MPENJA BLOG, Mpiganaji Baraka Adson Mpenja akitunukiwa cheti chake baada ya kuhitimisha semina hiyo kwa uaminifu mkubwa.
Carol Moshi alitunukiwa cheti leo hii
 Victoria Mhagama naye alitunukiwa cheti
Mwanamitindo anayekuja juu, Annastazia Gura naye alitunukiwa cheti baada ya kuhitimisha semina hiyo
 Bwana Okoka naye hakubaki nyuma
 Grace Boniface naye alitunukiwa cheti leo hii
Baada ya kutunuku vyeti , Dkt. Makoye hakusita kuwapongeza washiriki na kuwataka kutumia yale yote waliyojifunza kuendeleza taaluma zao.
PICHA ZOTE NA MPENJA BLOG

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video