Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MABADILIKO ya mfululizo katika benchi la ufundi imetajwa kuwa moja ya sababu
ya Wekundu wa Msimbazi kufanya vibaya msimu wa 2013/2014 uliomalizika aprili 19
mwaka huu kwa timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na watani zao wa Jadi, Yanga SC.
Simba walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 4
baada ya kujikusanyia pointi 38 pekee katika michezo 26.
Ally Mayay Tembele, beki na nahodha wa zamani wa
Yanga sc na sasa kocha wa mpira wa miguu amesema kuwa kubadili benchi la ufundi
mara kwa mara kunaleta athari ya moja kwa moja katika kikosi.
“Kila mwalimu ana falsafa yake, kwahiyo
unapobadili kocha ujue kabisa unaleta mfumo mpya katika klabu ambao utahitaji
muda ili wachezaji wazoee”.
“Msimu wa 2011/2012 alikuwepo kocha Mserbia
Milovan Circovic, baadaye akaja mfaransa Patric Liewig. Akiwa ameshaanza
kuijenga Simba ya vijana na sasa wanaanza kumuelewa, akaondolewa na kuletwa
Abdallah Kibadeni. Hawa ni walimu watatu tofauti na wana aina yao ya ufundishaji”
“Wachezaji ndani ya muda mfupi walijikuta wakilishwa
mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa haraka kwasababu wakianza kuzoea
kunatokea mabadiliko”
“Kibadeni alikuwa ameanza kuwaweka vijana wake
vizuri na tuliona Simba ikianza kutambulika na makinda wake, ghafla anatimuliwa
na analetwa Mcroatia Dravko Logarusic; Huyu naye ana mfumo wake”.
“Kwa mazingira haya, Simba isingeweza kutengamaa
kwa haraka na walihitaji muda sana”. Alisema Mayay ambaye pia ni mchambuzi wa
Soka.
Simba kwasasa wapo katika mazungumzo na kocha
Logarusic ili kuoana kama wanaweza kumpa mkataba mwingine.
Katibu mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema
hatima ya kocha huyo ni mwishoni mwa wiki hii’
Kamwaga alikaririwa akisema: “Simba tunamhitaji
Loga tofauti na watu wanavyodhani. Cha msinhgi ni kuwa kwasasa tuko katika
mazungumzo ya mkataba mpya. Mwishoni mwa wiki hii tutaweka mambo hadharani”.
Kocha Loga amekuwa akishutumiwa na wachezaji kuwa
anawabebesha mzigo mzito na ni mkali mno pale wanapohitaji busara zake.
Loga ni muumini mkubwa wa nidhanu na ana msimamo
mkali kwa wachezaji na viongozi wake.
Mara nyingi amekuwa akiwaadhinu wachezaji wake
uwanjani pale wanapofanya makosa.
Hauno shida kumkalisha mchezaji benchi au kumtoa
dakika yoyote ya mchezo kama anafanya uzembe tofauti na matarajio yake.
0 comments:
Post a Comment