Rais
wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Sepp Blatter ametuma salamu za
pongezi kwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC.
Blatter ameandika barua hiyo kwa
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na kutoa pongezi hizo.
Amewapongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutokana na kuweka rekodi
mpya ya bingwa tofauti.
Malinzi
amethibitisha kupokea barua hiyo ya Blatter na kusema atawakabidhi Azam FC,
kesho.
Aidha, Malinzi naye ametuma pongezi hizo za ubingwa kwa Azam FC.
“Tutawakabidhi barua hiyo ya Blatter kutoka Fifa, lakini
tunawapongeza kutokana na kutwaa ubingwa,” alisema Malinzi.
Pongezi za Blatter kwa Azam FC ni za kwanza kwa rais huyo wa
fifa kwa klabu iliyotwaa ubingwa Tanzania
0 comments:
Post a Comment