Monday, April 14, 2014


149Muhidini Gurumo (kushoto)  enzi za uhai alipopewa zawadi ya Gari na msanii maarufu wa Bongo Fleva nchini, Diamod Platinumz
……………………………………………………………………………………………….
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
imagesNational Arts Council BASATA
Yah: Salaam za Rambirambi
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini Maalimu Ngurumo
“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
  Imetolewa na
Godfrey Mngereza
Kaimu Katibu Mtendaji
Baraza la Sanaa la taifa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video