MAJANGA
BARCA!. Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa wiki nne,
wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote kupata majeruhi.
Klabu
ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata majeruhi ya mguu jana katika
mchezo wa fainali ya kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.
Kinda
huyo mwenye miaka 21 alishindwa kuisaidia Barca kuepukana na kipigo cha mabao
2-1, huku Mbrazil huyo akikosa nafasi ya wazi dakika za lala salama.
Neymar
atakosa mechi zijazo dhidi ya Athletic Bilbao, Villarreal, Getafe na Elche.
Hata
hivyo klabu ya Barca ina matumaini kuwa nyota wake huyo anaweza kurudi katika
mechi ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid.
Taarifa
ya klabu ya Barcelona imesema;”Mchezaji huyu aliumia jana katika mguu wake wa
kushoto na anahitaji muda maalumu wa matibabu. Makadirio ya kurudi uwanjani ni
wiki nne”.
Naye
Jordi Alba alitolewa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mechi ya
jana na taarifa zinaeleza kuwa beki huyo wa kushoto aliumia nyama za paja za
mguu wake wa kulia.
Beki
huyo wa zamani wa Valencia anaweza kukaa nje ya uwanja kwa wiki tatu hadi nne.
0 comments:
Post a Comment