Thursday, April 10, 2014

Baada ya kutolewa hatua ya Robo fainali na Atletico Madrid, beki wa kulia wa FC Barcelona, Dan Alves ametoa kisingizio kuwa wameshindwa kutamba kutokana na  uwanja wa  Vicente Calderon kuwa katika hali mbaya.

Barca walipoteza mechi  kwa bao  1-0  baada ya  Koke kufunga bao dakika tano za mwanzo, hivyo wastani wa mabao kuwa 1-1 kufuatia sare ya 1-1 kwenye  mechi ya kwanza uwanja wa Camp Nou.

Dani Alves baada ya mechi amelalamikia hali ya uwanja kuwa ulikuwa na nyasi ndefu na unyevu baada ya mapumziko.

Amelieleza gazeti la Marca kuwa : "Haikuwa rahisi kushinda mechi ya jana, Atletico Madrid walicheza na silaha zote, na waliacha uwanja katika hali mbaya".

"Uwanja haukuwa mzuri na ulipunguza kasi ya mpira. Kwa mpango huo, waliweza kutushinda kwa kupiga mipira mirefu na mashambulizi ya kushitukiza."

Mbrazil huyo alishindwa kuisadia timu yake kushinda katika michezo yote miwili, hata hivyo aliongeza kuwa;

"Kiukweli jana wameshinda kihalali. Pale timu pinzani inapofanya vizuri inabidi kuwapongeza. Kila kilichotokoea uwanjani kilikuwa sahihi".

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video