Na Francis Godwin Blog
WAKATI macho na masikio ya watanzania yakielekezwa bunge la Katiba mjini Dodoma kuona Tanzania inapata katiba mpya ,Askofu maarufu na mtabiri wa mambo mbali mbali nchini Dr Boaz Sollo (pichani )wa kanisa la Overcomers Power Centre Iringa ametangaza kufunga na kuomba kwa ajili ya kuliombea bunge la katiba ili wajumbe kufanya maamuzi bila kukwazana.
WAKATI macho na masikio ya watanzania yakielekezwa bunge la Katiba mjini Dodoma kuona Tanzania inapata katiba mpya ,Askofu maarufu na mtabiri wa mambo mbali mbali nchini Dr Boaz Sollo (pichani )wa kanisa la Overcomers Power Centre Iringa ametangaza kufunga na kuomba kwa ajili ya kuliombea bunge la katiba ili wajumbe kufanya maamuzi bila kukwazana.
Dr Sollo ambae amepata kutoa utabiri wake mwishoni mwa mwaka jana kuwa watanzania kwa mwaka huu watapata neema kubwa ya mvua na kutokea kwa mafuriko mkoani Morogoro pamoja na maeneo ya ukame kama Isimani kuwa na mvua ,alisema kuwa anatabiri neema ya katiba bora iwapo watanzania watazama katika maombi ya kuliombea Taifa .
Akizungumza na waandishi wa habari hizi jana kuhusu maombi hayo ya opresheni ya kutokomeza uchawi na laana pamoja na kuliombea bunge la katiba ,askofu Dr Sollo alisema kuwa mbali ya watanzania waliowengi kuonyesha kukata tamaa juu ya mwenendo wa wajumbe wa bunge la katiba mjini Dodoma kutokana na marumbano yasiyo kwisha ila bado imani ya Rais Dr Jakaya Kikwete kuona mchakato huo wa katiba unamalizima kwa kuwa na katiba bora .
Kwani alisema kuwa wajibu wa kanisa lake na viongozi wengine wa dini ni kuwaelekeza waumini wao katika maombi zaidi ili kuwaombea wajumbe wa bunge hilo la katiba ili kufanya maamuzi ya msingi katika kuiandaa katiba hiyo pasipo kutanguliwa na jazba yoyote .
” Nchi yetu ina idadi ya watu zaidi ya milioni 40 na wajumbe waliopo bungeni Dodoma ni chini ya watanzania 1000 hivyo ni imani ya watanzania waliowengi kuona wajumbe hao wanaifanya kazi hiyo ya wengi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa na kila uamuzi watakaoufanya ni lazima kumtanguliza Mungu ili ashushe baraka zake”
Hata hivyo alisema kuwa si wakati wa wajumbe wa bunge hilo la katiba kuanza kurumbana kwa hotuba ya Rais Dr Kikwete wakati wa uzinduzi wa bunge hilo badala ya kuifanya kazi iliyopo mbele yao ya kuipitia rasmu ya katiba na kuandaa katiba ya watanzania .
Alisema akiwa ni kiongozi wa kanisa la Overcomers Power Centre Iringa anatambua mchango mkubwa wa viongozi wa Taifa hili chini ya Rais Dr Kikwete ambae ameweza kuiongoza nchi kwa hali ya amani na utulivu na hata wananchi wake wakiendelea kutumia uhuru wao wa kuabudu tofauti na nchi nyingine ambazo kila kukicha ni machafuko ya kitini na kisiasa .
“Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa kulijaria mema Taifa la Tanzania chini ya kiongozi wake Rais Dr Kikwete ……wajibu wetu kama kanisa la Overcomers Power Centre Iringa na wajibu wa viongozi wote wa dini na waumini wao ni kuendelea kuliombea Taifa “alisema askofu Dr Sollo
Akielezea kuhusu utabiri mbali mbali ambao amepata kuufanya ukiwemo wa neema ya mvua kwa Taifa kwa mwaka huu na machafuko ya nchi za jirani askofu Dr Sollo alisema amekuwa akiyafanya hayo kutokana na maono mbali mbali ambayo Mungu amekuwa akimuonyesha wakati wote na hivyo hataacha kuwaeleza watanzania maono mbali mbali atakayoonyeshwa .
Katika hatua nyingine askofu Dr Sollo ameeleza mafanikio makubwa ambayo Mungu ameendelea kulijalia kanisa lake hasa katika kufanikisha ujenzi wa kanisa la Kisasa ujenzi unaoendelea eneo la Zizi la Ng’ombe kwa nguvu za waumini wa kanisa hilo na wa nje ya kanisa hilo ambao wamekuwa wakifurahishwa na huduma ya maombezi inayofanyika na kuwa kamwe siku zote mbali ya kumshukuru Mungu kwa kazi hiyo ila bado ataeneza mbegu ya amani na upendo kwa watanzania .
0 comments:
Post a Comment