
ARSENAL wameendelea kujiongezea matumaini ya kuingia timu nne bora msimu huu baada ya ushindi wa mabao 3-0 jioni hii dhidi ya wana fainali wenzao wa kombe la FA, Hull City kwenye uwanja wa KC.
Mjerumani, Lukas Podolski amefunga mabao mawili katika dakika ya 45 na 53, lakini Aaron Ramsey ndiye alikuwa wa kwanza kuandika bao
la kwanza katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza, na kuwafanya Asernal
wawe juu ya Everton bila kujali matokeo ya mechi inayoendelea muda huu
Goodison Park kati ya Everton na Manchester United.
Hull
walicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini bao la pili la Podolski
katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili liliwachanganya na sasa
wanahitaji kujipanga zaidi kabla ya kukutana na Asernal mwezi ujao.
Baada
ya ushindi wa huu, Asernal wanafikisha pointi 70 katika nafasi ya 4,
wakati wapinzani wao Everton waliopo nafasi ya 5 kwa pointi 66 wapo
uwanjani kuumana na Man United.
Ramsey
amerejea leo baada ya kukaa nje ya uwanja wa muda mrefu kutokana na
majeruhi, na urejeo wake umekuwa na faida kwa timu kwasababu amecheza
mpira mzuri na kufunga bao muhimu.
Naye Mesut Ozil ambaye hajacheza tangu machi 11 ameonekana leo na kuonesha soka zuri.
Ushindi
huu ni muhimu kwa kocha Asernal Wenger kwasababu ndoto zake ni kutafuta
nafasi ya nne ili kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.
Asernal
walianza ligi vizuri na kuongoza kwa muda mrefu, lakini walianza
kupoteza mwelekeo na hatimaye kuwaachia Liverpool, Chelsea na Man City
waendeleze vita ya ubingwa.
0 comments:
Post a Comment