MATUMAINI ya Asernal kufuzu kucheza ligi ya mabingwa barani
Ulaya msimu ujao yameanza kufufuka baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
dhidi ya West Ham kwenye mchezo wa ligi kuu soka nchini England uwanja wa Emirates.
Lukas Podolski amefunga mabao mawili katika dakika ya 44 na 78, huku moja likifungwa na Olvier Giroud dakika ya 54.
Westham walikuwa wa kwanza kufunga leo hii katika dakika ya 40 kipindi
cha kwanza kupitia kwa Matthew Jarvis .
Mashabiki wa Asernal huwa hawana imani kubwa na Giroud na katika
mchezo wa leo alikosa nafasi kadhaa kipindi cha kwanza, lakini wakati mashabiki
wakijiuliza kama mshambuliaji huyo anaweza kuwa tegemeo kwa siku za usoni,
alifunga bao muhimu mno katika ushindi huo.
Umuhimu wa bao la Giroud unatokana na uhitaji mkubwa wa Asernal
kufuzu michuano ya UEFA msimu ujao.
Kikosi hicho cha Aserne Wenger kilianza vizuri ligi na kuongoza kwa
muda mrefu, lakini mambo yakabadilika ghafla na kuwapisha wanaume Chelsea, Man
City na Liverpool ambao wanachuana mpaka sasa.
Sasa Wenger na vijana wake wapo katika hatari ya kushindwa kufuzu
UEFA kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 17 baada ya kuwapisha Everton katika
nafasi ya nne kwa muda.
Lakini baada ya kushinda mechi ya leo dhidi ya wapinzani wao wa
London, Asernal wamerejea nafasi ya nne kwa kufikisha pointi 67, huku Everton
wakishuka mpaka nafasi ya tano kwa pointi zao 66, lakini kesho wanacheza dhidi
ya Crystal Palace.
Asernal Wenger baada ya mchezo amesema kuwa walikuwa katika
presha kubwa ya kushinda mchezo, lakini ilikuwa mechi ngumu mno.
“Niliridhishwa na ukomavu wa timu yangu. Walionesha kutulia
baada ya kufungwa bao la kwanza”.
“Kazi kubwa ilikuwa kusawazisha bao kabla ya mapumziko. Ilikuwa
vita kubwa na ilikuwa ya kufurahisha”. Alisema Wenger.
0 comments:
Post a Comment