CARLO
Ancelotti anaamini kuwa hali ya hewa iliyopo Real Madrid kwa sasa inatosha
kuwapa ushindi dhidi ya Bayern Munich kesho kutwa (jumanne) kwenye nusu fainali
ya pili ya UEFA uwanja wa Allianz Arena.
Ancelloti
aliiongoza Real Madrid kuifunga bao 1-0 Bayern kwenye nusu fainali ya kwanza
uwanja wa Santiago Bernabeu wiki iliyopita na bao hilo pekee lilifungwa na mfaransa,
Karim Benzema.
Madrid
walipasha moto misuli yao jana kwa kuifunga Osasuna mabao 4-0 kwenye mchezo wa
La Liga na mabao hayo yalifungwa na Sergio Ramos, Daniel Carvajal na `Mnyama`
Cristiano Ronaldo alipiga mawili.
“Ni
wazi kujua hali ya hewa iliyopo sasa katika klabu na mashabiki wake”. Alisema
Ancelotti mwenye miaka 54.
“Kama
nisemavyo mara kwa mara, hii ni muhimu, ni muhimu kuwa na hali kama hii
kuelekea mechi zijazo”.
Los
Blancos (Real Madrid) wanapigania kuchukua kombe la UEFA kwa mara ya 10 tangu
walipofanya hivyo mwaka 2002 walipoifunga mabao 2-1 Bayern Leverkusen.
Ancelotti
amekaririwa akisema kwa kikosi chake cha sasa anataka kuwa meneja wa kwanza kuiongoza
Real Madrid katika harakati zake za kuchukua kombe la UEFA kwa desimali mbili
yaani 10.
“Kila
mtu anasubiri kuona nini kitatokea na kwa mawazo haya klabu inaweza kufanya
vizuri. Alisema Carlo.
“Kikosi
nitakachopanga mjini Munich ni kile cha wachezaji wapambanaji. Kwasasa
hatutafanya mabadiliko yoyote kuhusiana na mchezo huo”.
“Kila
mtu awe mtulivu kwasababu tunajiandaa vizuri juu ya mechi hii. Nawaamini
wachezaji wangu na nadhani kila mtu awaamini”. Aliongeza Carlo.
0 comments:
Post a Comment