CARLO Ancelotti amesema Real Madrid inahitaji
kufunga mabao katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi ya Bayern Munich leo Allianz
Arena.
Los Blancos (Real Madrid) wataingia uwanjani
wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0 walilofunga kupitia kwa Karim Benzema katika mchezo
wa kwanza uwanja wa Santiago Bernabeu.
Lakini Ancelotti amesisitiza kuwa licha ya timu
yake kuwa na faida ya bao moja si sababu ya kuingia kwa kulinda na
ameshawaambiwa wachezaji wake kuonesha dhamira ya kucheza fainali baada ya
kupita zaidi ya muongo mmoja.
“Inawezekana kufuzu bila kufunga, lakini dhamira
yetu ni kufunga.”.
“Tumefunga mabao mengi UEFA na La Liga na
tunahitaji kufanya hivyo tena”. Ancelotti amewaambiwa waandishi wa habari.
“Tunaweza kucheza mifumo tofauti ya mpira, lakini
kwa michezo mingi tunajaribu kushambilia “
“ Tutatumia faida ya kuwa na wachezaji walioimarika
kimaumbo na kiufundi”.
“Tunajua mechi ya leo itakuwa ngumu sana.
Tunacheza na timu kubwa tukiwa na faida ndogo, kwahiyo sisi sio wapumbavu na
kamwe hatuwezi kuingia kwa kudhani tayari tumeshafuzu”.
Naye Kocha wa Bayern Munich, Josep Pep Guardiola
amesema malengo yake ni kupindua matokeo ya kwanza na kusonga hatua ya fainali.
Gaurdiola alikiri ugumu wa mchezo huo, lakini
alisema wameshajiandaa kushinda.
“Mimi nataka kushinda. Wachezaji wanataka kushinda
na mashabiki wanataka kushinda”
“Kwa matarajio kama haya, lazima tuingie kwa nguvu
moja”.
“Najua Real Madrid ni timu kubwa na siku zote
nafurahi kucheza nusu fainali hasa na klabu kama hii. Itakuwa mechi ngumu lakini
tutajitahidi kupata matokeo”. Alisema Gaurdiola.
0 comments:
Post a Comment