KOCHA
wa Real Madrid, raia wa Italia, Carlo Ancelotti ameutetea mfumo
aliotumia Pep Guardiola wakati klabu yake ilipopambana na Bayern Munich
katikati ya wiki na kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Guardiola raia wa Hispania
alikosolewa kwa mfumo wake aliotumia jumatano ya wiki hii ambapo timu
yake ilifurahia kumiliki mpira, lakini iliambulia kichapo.
Kocha huyo wa zamani wa FC
Barcelona tayari ameshabeba taji la Bundesliga msimu huu, lakini
Ancelotti amesema ana mfumo mzuri na sasa hawezi kuzungumza lolote zaidi
ya kuangalia mchezo wa kesho wa La Liga dhidi ya Osasuna
“Napenda mfumo wa Guardiola. Alileta mfumo mpya katika mpira. Ana aina ya mpira wake”. Ancelotti amewaambiwa waandishi.
“Nampenda sana mfumo wa Pep,
ameleta aina yake ya mpira, alitumia akiwa Barca na sasa anautekeleza
akiwa Bayern, japokuwa kuna ugumu kwake”.
“Bayern imefanikiwa na kocha
wake. Pep anafanya kazi nzuri. Lakini bado hatujaanza kufikiria mechi ya
Munich kwasababu mechi ya kesho ni muhimu kwetu”.
Ancelotti amekuwa akihusishwa na
taarifa za yeye kujiunga na Manchester United kufuatia kutimuliwa kwa
David Moyes, lakini kocha huyo wa zamani wa Chelsea amesema hafikirii
kuondoka Santiago Bernaberu kwa sasa.
“Kila mwaka haya yanatokea na nazungumza kitu kile kile. Nina furaha kuwepo hapa”.
“Najiona mwenye bahati kuwa na
moja ya klabu bora zaidi duniani. Nawaheshimu Man United na kile
kilichomtokea Moyes, lakini nipo hapa”. Alisema Ancelotti.
Ancelotti ataiongoza Madrid Allianz Arena jumanne ya wiki ijayo, baada ya mechi ya kesho ya La Liga dhidi ya Osasuna.
Ataingia katika mechi hiyo nusu
fainali ya pili ya UEFA akiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 na
atahitaji kuulinda ushindi huo ili kukutana nna Chelsea au Atletico
katika mchezo wa fainali mei 24 mwaka huu mjini Lisbon nchini Ureno.
0 comments:
Post a Comment