UNAPOZUNGUMZIA wachezaji wa Kitanzania wenye bahati
ya kucheza klabu kubwa duniani, huwezi kuacha kumzungumzia Adam Nditi
anayekipiga katika klabu ya Chelsea.
Nditi amepata bahati ya kunolewa na kocha bora
duniani, Jose Mourinho katika dimba la Stamford Bridge.
Mahojiano maalum yamefanywa baina ya mtandao huu
na Nditi akiwa jijini London nchini Uingereza.
Nditi amefafanua kuwa katika mazoezi wanayofanya
chini ya kocha Mourinho wanafundishwa mambao matatu.
“Katika mazoezi yetu, tunafundishwa namna ya kulinda, kucheza na
kufunga”
“Kocha anatumia muda mwingi katika masuala haya
matatu”.
“Kila klabu ina mbinu zake za kusaka ushindi
katika mechi”. Amesema Nditi.
Aidha, kinda huyo alishangazwa na maneno ya watu
kuwa walicheza kwa kujilinda zaidi “maarufu kama kupaki basi `dhidi ya Liverpool
jumapili iliyopita na kushinda mabao 2-0 kwenye uwanja wa Anfield.
“Watu wanasema tulipaki basi, sasa ilikuwaje
tukafunga mabao mawili?, au Liverpool walijifunga?, kila timu ina mbinu zake za
kutafuta matokeo”.
“Timu yetu ilijilinda ili isifungwe, ikacheza
mpira na kushambulia na kupata mabao mawili”.
“Nilisema toka awali kuwa kocha Mourinho
anatufundisha kulinda , kucheza mpira na kushambulia ili tufunge”.
“Tulifanya vyote, tulilinda lango letu, tukacheza
mpira na kufunga”
“Hii ni mbinu ya Chelsea na kocha wetu, Jose
Mourinho”.
Akiuzungumzia mchezo wa kesho kutwa dhidi ya
Atletico Madrid katika nusu fainali ya pili ya ligi ya mabingwa barani Ulaya,
Nditi alisema wanajiamni kuibuka na ushindi.
“Mechi na Atletico timu itabadilika kiuchezaji,
Usitegemee kuona mpira uliochezwa Hispania, hapa nyumbani tutacheza tofauti na
kupata ushindi”. Amesema Nditi.
Chelsea katika mchezo wa kwanza ulilazimisha
suluhu pacha ya bila kufungana na Atletico katika dimba la Vicente Calderon na
ili kufuzu hatua ya fainali wanatakiwa kushinda bao 1-0.
Hii itakuwa mechi muhimu kwa Jose Mourinho mwenye
chagizo la kushinda mchezo mgumu wa ligi dhidi ya Liverpool jumapili iliyopita.
0 comments:
Post a Comment