Wachezaji wa Young Africans wakiwasili katika Hoteli
ya Sheraton
....................................................................
Msafara wa
kikosi cha Young Africans umewasili salama jijini Alexandria leo majira ya saa
7 na kufikia katika hoteli ya Shaeraton ukitokea katika jiji la Cairo ambako
awali mchezo wa marudiano ulipangwa kufanyikwa kabla ya jana kutolewa
mabadiliko ya uwanja na mchezo huo utachezwa kesho katika dimba la Uwanja wa El
Max Stadium jijini Alexandria.
Young
Africans ambayo iliwasili juzi jijini Cairo na kuweka kambi katika hoteli ya
Nile Paradise Inn na kufanya mazoezi kwa siku mbili mfululizo katika uwanja
uliopo ndani ya hoteli hiyo ambayo uongozi wa Young Africans kwa kushirikiana
na Ubalozi uliweza kufanikisha kambi hiyo.
Awali makamu
mwenyekiti wa Young Africans Clement Sanga alitangulia jijini Alexandria jana
asubuhi pamoja na maofisa wa ubalozi kwa ajili ya kufanya maaandalizi ya sehemu
ambapo timu itafikia na leo timu ilipofika ilikuta kila kitu kmeshakaa kwenye
mpangilio wake.
Mara baada ya
kuwasili jijini Alexandria wachezaji na viongozi wa Young Africans wamepata
chakula cha mchana kisha wamepata mapumziko mpaka majira ya saa 12 jioni ambapo
timu itakwenda uwanja wa El Max kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea
kwenye mchezo huo.
Morali
ya wachezaji bado ni ya hali ya juu kuelekea mchezo huo wa kesho, haki ya kambi
ni nzuri hakuna majeruhi hata mmoja hivyo vijana wote wapo tayari kwa
kesho kuipeperusha bendera ya nchi.
Jioni timu
itafanyya mazoezi katika Uwanja wa El Max ambao ndio utakaotumika kwa mchezo wa
kesho.
0 comments:
Post a Comment