Na Baraka Mpenja
0712461976 au 0764302956
BAHATI haikuwa kwa Yanga usiku huu. Wametolewa na Al
Ahly kwa mikwaju ya penati katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani
Afrika kuwania hatua ya 16 bora baada ya kufungwa bao 1-0 ndani ya dakika 90.
Mabingwa watetezi, National Al Ahly
wamepata penati 4 huku Young Africans
wakipata penati 3.
Waliofunga penati za Yanga ni Didier Kavumbagu `Kavu`, nahodaha na beki wa
kati, Nadir Haroub `Canavaro`, na
Emmanuel Anord Okwi .
Wanandinga wa Yanga waliokosa penati
usiku huu ni Oscar Samwel Joshua , Said Bahanuzi na Mbuyu Twite .
Mlinda mlango namba moja wa Yanga
Deogratius Munishi ‘Dida’ alipangua penalti mbili mfululizo ya nne na ya tano,
lakini Yanga SC nao wakakosa penalti mbili mfululizo ya nne na ya tano.
Mbali na kupangua penati hizo,
alicheza vizuri ndani ya dakika 90 na kuwa kikwazo kikubwa kwa Al Ahly kupata
ushindi.
Mchezo wa leo umemalizika kwa Yanga
kufungwa bao moja sawa na matokeo waliyoyapata Yanga katika mechi ya kwanza
jijini Dar es salaam, Machi mosi mwaka huu uwanja wa Taifa.
Bao la Alhly ndani ya dakika 90 lilifungwa
katika dakika ya 70 na baada ya hapo liliwaamsha zaidi wenyeji hao na kuongeza
mashambulizi katika lango la Yanga.
Yanga walipata nafasi za kufunga
katika dakika ya 54 kipindi cha pili ambapo winga mwenye kasi kubwa, Simon
Msuva alikosa umakini.
Dakika ya 89, Frank Domayo `Chumvi`
aliikosesha Yanga bao la kusawazisha baada ya kushindwa kutumia nafasi
aliyoipata.
Kipindi cha kwanza Waarab walikuwa golini kwa Yanga kwa muda
mwingi, huku Yanga wakifanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini dakika 45 za
kipindi cha kwanza zilimalizika bila kufungana.
Yanga walihitaji sare au suluhu,
kama si hivyo kufungwa kwa toafauti ya bao moja, ,mfano, 2-1, 3-2 ili kusonga
mbele ndani ya muda wa kawaida.
Kufungwa bao moja kumewalazimu
kwenda hatua ya penati ambayo huwa ni bahati tu na si ufundi muda mwingine.
Matokeo ya Yanga yamewaumiza
mashabiki, wanachama, viongozi, benchi la ufundi na watanzania kwa ujumla, kwani
wao ndio walibaki wawakilishi pekee wa nchini katika michuano ya ligi kuu.
Kwasasa Timu zote za Tanzania
zimetolewa katika mashindano ya Kimataifa.
Poleni sana wana Yanga kwa matokeo
hayo, huo ndio mpira. Jipangeni upya na mrudi ligi kuu ili mtetee ubingwa wenu
na kushiriki tena mwakani.
0 comments:
Post a Comment