Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
HATIMAYE Al
Ahly wametaja uwanja utakaotumika katika mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya
mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye
mashindano ya kimataifa, Dar Young Africans.
Shirikisho la soka nchini Misri limesema kuwa mchezo
huo wa jumapili machi 9 mwaka huu utafanyika
mjini Alexandria katika Uwanja wa Border Guard stadium (Haras el Hadod) .
Awali mchezo huo ulitakiwa kufanyika mjini Cairo na sasa utafanyika katika mji wa
Alexandria takribani kilometa zaidi ya 200 kutoka Cairo ambapo kikosi cha Young
Africans kimeweka kambi kujiandaa na mchezo huo.
Taarifa kutoka kwa viongozi wa Yanga wakiongozwa na
makamu mwenyekiti wake C iment Sanga imeleza kuwa baada ya kupewa taarifa kupitia
Ubalozi wa Tanzania nchini Misri, tayari wameanza maandalizi ya kuhakikisha
timu inakwenda mjini Alexandria kucheza mchezo huo wa jumapili na kufanya
vizuri.
Hata hivyo Yanga wameshangazwa na taarifa za Uwanja kutolewa siku tatu kabla ya mchezo huku wahusika
wakitambua kuwa Young Africans ilifahamu mchezo huo utafanyika Cairo takribani
wiki mbili zilizopita na viongozi wa Al Ahly waliopokuwa nchini Tanzania
walidhibitisha hilo.
Sehemu ya taarifa hiyo imesema kuwa “Pamoja na mabadiliko hayo ya ghafla ya sehemu
utakapofanyika mchezo siku ya jumapili, benchi la ufundi pamoja na wachezaji na
viongozi waliopo jijini Cairo bado wana imani ya kufanya vizuri na kusonga
mbele katika hatua ya 16 bora”.
Wakati hayo yakijiri, nao washambuliaji wa Yanga raia
wa Uganda, Hamisi Kizza na Emmanuel Okwi tayari wameshawasili jijini Cairo usiku
wa jana majira ya saa 7 kwa shirika la ndege la Egypt Air wakitokea nchini
Zambia walipokuwa wakiiwakilisha timu yao ya Taifa kwenye mchezo wa kirafiki
siku ya jumatano dhidi ya Zambia na The Cranes kulala kwa mabao 2-1.
Katika mchezo huo uliopigwa mjini Lusaka, bao la
Uganda lilifungwa na Hamis Friday Kiiza na .
Mchezo huo wa siku ya jumapili ambao unafanyika mjini
Alexandria katika Uwanja wa Border Guard Stadium (Haras El Hadod) hautakua na
watazamaji kutokana na mamalaka ya ulinzi na usalama kuzuia mashabiki kuingia katika
mchezo wowote wa mpira wa miguu nchini Misri.
Yanga wataingia uwanjani wakiwa na faida ya ushindi
wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa machi mosi , uwanja wa Taifa jini Dar es
salaam.
Bao pekee la Yanga lilifungwa katika dakika ya 82 na
beki wa kati na nahodha wake,Nadir Haroub `C
Canavaro` kwa njia ya kichwa.
Inafahamika kuwa Waarabu wana fitina sana wanapokuwa
nyumbani kwao, lakini umoja wa Yanga na kujituma kwa wachezaji wao ndio itakuwa
silaha pekee ya kuwaangusha wenyeji wao.
Yanga wanahitaji sare au suluhu katika mchezo huo, au
kama wanafungwa basi wafungwe kwa tofauti ya bao moja mfano; 2-1, 3-2 ili
wanufaike ba bao la ugenini.
Al Ahly wataingia uwanjani kwa lengo la kutafuta
mabao zaidi, lakini Yanga watatakiwa kuwa makini muda wote wa mchezo hasa
dakika za kwanza ili wasifungwe mapema na kuvurugwa zaidi.
Kila mchezaji wa Yanga anatakiwa kufahamu kuwa
watanzania wapo nyuma yao wakiwaombea dua, cha msingi wafanye kazi yao kwa
bidii ili kubadili historia ya udhaifu wa Yanga kwa timu za kaskazini mwa
Afrika.
Mtandao huu unawatakia kila la heri Yanga katika
mchezo huo mkubwa wa jumapili.
0 comments:
Post a Comment