Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0712461976 au 0764302956
MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara,
Young Africans wameweka kambi makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya
Twiga na Jangwani, jijini Dar es Salaam kujiwinda na mchezo wa kesho kutwa (jumatano) wa ligi kuu dhidi ya maafande wa
Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Yanga imeanza mazoezi yake jioni ya
leo chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Hans Van Der Pluijma akisaidiwa na Mzalendo,
Charles Boniface Mkwasa `Master`.
Wakati huo huo, Prisons wamewasili jijini
Dar es salaam jioni ya leo wakitokea Mkoani Morogoro walipoweka kambi yao.
Katibu mkuu wa Wajelajela hao, Inspekta
Sadick Jumbe amesema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekwenda vizuri na
wamefika mapema ili kesho wajiweke sawa tayari kwa shughuli ya jumatano.
“Yanga wanaonekana kuwa na mikakati mizito juu
yetu kwasababu ya misemo yetu ya `Hatoki mtu hapa` na `moto hauzimwi kwa petroli`.
Kweli lazima waogope kwani tumejipanga kuchukua pointi tatu”. Alisema Jumbe.
Jumbe aliongeza kuwa kwasasa
wanahitaji pointi zaidi ya nne katika michezo yao iliyosalia, hivyo Yanga
lazima wajipange vizuri.
“Niwaombe mashabiki wetu kuwa na imani
na kikosi chetu. Tumejipanga vizuri na wajitokeze kuishangilia timu yao hapo
kesho kutwa”. Alisema Jumbe.
Prisons wapo nafasi ya 10 wakiwa
wamejikusanyia pointi 22, huku Yanga wakiwa nafasi ya pili kwa kujikusanyia
pointi 43.
Mbeya City wapo nafasi ya tatu kwa
pointi 42 na nafasi ya nne inakaliwa na Simba wenye pointi 36.
0 comments:
Post a Comment