Na Mtandao rasmi wa Yanga
Kikosi cha wa waliokuwa wawakilishi pekee wa mashindano ya
kimataifa nchini Tanzania Young Africans kinatarajiwa kuwasili kesho alfajiri
jijini Dar es salaam kwa shirika la ndege la Egypt Air kikitokea jijini Cairo
nchini Misri kilipokuwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly na kutolewa kwa
mikwaju ya penati 4-3 mchezo uliofanyika katika Uwanja wa El Max jijini
Alexandria.
Mara baada mchezo huo uliofanyika siku ya
jumapili na wenyeji kufuzu hatua ya 16 kwa mikwaju ya penati, msafara wa
viongozi wa Young Africans pamoja na wachezaji waliwasili jana mchana jijini
Cairo na kufikia katika hoteli ya Marriot iliyopo eneo la Zamalek.
Balozi wa Tanzania nchini Misri Bw Mohamed
Hamza aliandaa chakula cha jioni kilichojuimsha wachezaji, viongozi, maofisa
ubalozi na familia zao, waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watanzania
waishio nchini Misri.
Akiongea kwa niaba ya serikali Balozi
Hamza aliwaambia wachezaji wasivunjike moyo kwani wamepambana kadri ya uwezo
wao, timu ilicheza vizuri lakini mwisho wa siku bahati haikuwa yao hivyo
wajipange upya ili mwakani waweze kufanya vizuri zaidi ya mwaka huu.
Leo asubuhi kikosi cha Young Africans
kilifanya mazoezi katika uwanja wa Al Ahly uliopo makao makuu ya klabu hiyo
eneo la Zamalek kisha mara baada ya mazoezi viongozi walipata fursa kuongea na
viongozi wa Al Ahly wakiwemo makocha ambao walitoa pongezi kwa wachezaji wa
Yanga kwa kiwango walichokionyesha katika michezo yote miwili.
Uongozi wa Yanga unawashukuru
wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wote wa soka waliokuwa pamoja katika
kuiombea timu ya Yanga kufanya vizuri katika mchezo ambao vijana walitolewa kwa
mikwaju ya penati, wasivunjike moyo nguvu zote zinaelekezwa kwenye Ligi Kuu ya
Vodacom siku ya jumamosi dhidi Mtibwa Suga ya Morogoro lengo la uongozi na
wachezaji ni kutwaa Ubingwa wa VPL kwa msimu wa pili mfululizo.
0 comments:
Post a Comment