VIEWED 225 TIMES

Kikosi cha Young Africans Sports Club
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans
kesho watashuka dimbani kucheza na timu ya Mgambo JKT kutoka mjini
Handeni katika muendelezo wa michezo ya VPL 2013.14 kipute
kitakachofanyika kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Young Africans ambayo ilisawali jana mchana jijini Tanga na kufanya
mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Galanos jioni kabla ya leo
timu kufanya mazoezi asubuhi katika dimba la mkwakwani ambapo pia
washabiki walijitokeza kwa wingi kuiona timu hyo yenye wachezaji wenye
kiwango cha hali ya juu.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi
Hans Van der Pluijm amesema anashukuru timu ilifika salama jijini Tanga
na vijana wake wote kuweza kufanya mazoezi kwa siku mbili pasipo kuwa na
majeruhi wala mchezaji mwenye tatizo lolote.
"Uwanja wa Mkwakwani
sio mzuri hasa kwenye sehemu ya kuchezea kutokana na kuwa na mashimo
mashimo hivyo mara nyingi mipira hudunda na kuwapita wachezaji,
tumeliona hilo na kuwaeleza vijana wawe makini naamini kesho wakicheza
na Mgambo watakua makini na kutumia nafasi watakazozipata kuweza kuibuka
na ushindi" alisema Hans.
Mchezo wa kesho ni muhimu kwa Young
Africans kuweza kuibuka na ushindi kwani pointi 3 katika mchezo huo,
zitawafanya watoto Jangwani kufikisha alama 49 na kuwa na tofauti ya
pinti 1 dhidi ya Azam FC wanaongoza ligi.
Wapenzi, wanachama na
washabiki wa Young Africans manombwa kujitokeza kwa wingi kesho Uwanja
wa Mkwakwani kuja kuwapa sapoti vijana katika mchezo huo muhimu.
0 comments:
Post a Comment