Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Tanzania, Mwinda Kiula Mfugale akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Kansa ya Ocean Road, Sr. Genoviva Mlawa (kushoto), vilivyotolewa na wanawake wafanyakazi wa benki hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni baadhi ya wanawake haoMmoja wa maofisa waandamizi wa Benki ya NBC, Sarah Laizer , akikabidhi jora la khanga kwa Msaidizi wa Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Kansa ya Ocean Road, Sr. Genoviva Mlawa (kushoto) pamoja na vitu vingine vilivyotolewa na wanawake hao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Baadhi ya wafanyakazi wanawake hao wakiandaa khanga tayari kwenda kuwakabidhi wagonjuwa wanawake waliolazwa katika hospitali hiyo.Haikuwa Dar es Salaam pekee kwani hapa wafanyakazi wa Benki ya NBC Mkoani Singida nao walitembelea katika Hospitali ya mkoa huo na kwenda kutoa aina mbalimbali za misaada.Hapa wakibeba gunia la unga tayari kwenda kutoa msaada kwa wagonjwa wanawake waliolazwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuonyesha upenda na kuwajali wanawake wenzao walio katika shida. Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya NBC, wakipiga picha pamoja na Muuguzi Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Ocean Road , Dar es Salaam walipokwenda kuwatembelea wagonjwa wanawake waliolazwa katika hospitali hiyo na kuwapa aina mbalimbali za misaada kama sehemu ya maadhimisho aya Siku ya Kimataifa ya Wanawake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Home
»
»Unlabelled
» WANAWAKE WAFANYAKAZI WA NBC WAWAKUMBUKA WANAWAKE WENZAO WENYE MATATIZO
Monday, March 10, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment