Tuesday, March 11, 2014

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.


Wanafunzi wa shule ya Msingi Mwakikonge, wilayani Mkinga wanasomea chini ya miti ya mikorosho kutokana na kukosekana kwa madarasa shuleni hapo.


Shule hiyo yenye wanafunzi 450 ina madarasa mawili, walimu wanne na haina nyenzo muhimu za kufundishia tangu ilipoanzishwa mwaka 2009. 

Akizungumza katika mahojiano na NIPASHE, Diwani wa Kata ya Duga, Ali Ali, alisema wanafunzi wa shule hiyo walianza kusoma chini ya mti na mpaka sasa wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la tano wanasoma chini ya mti na darasa la sita na la saba tu ndio waliopo madarasani. 

“Hii shule inakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwamo ukosefu wa madarasa na walimu….walimu waliopo ni wanne tu na madarasa ni mawili tu na mwaka huu tuna  wanafunzi wa darasa la saba tangu shule ilipoanzishwa hatujui matokeo yatakuaje," alisema Ali. (UNAWEZA KUCHUKUA HII KAMA QUATATION)

Hata hivyo, wananchi wa Sweden kupitia mfuko wa Agape Charity, wametoa msaada wa vitabu vya masomo mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 6.8.

Mwakilishi wa Agape ni kwamba Charity, Clemeny Hongole, alisema vitabu hivyo ni vya masomo ya Kiswahili, Historia, Jiografia, Uraia, Stadi za kazi na kiongozi cha mwalimu kwa masomo yote.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video