Monday, March 24, 2014

01Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Richard Kasuga akiwaeleza waandishi wa habari  kuhusu tahadhari ya kutokea viwavi jeshi hapa nchini hivyo wananchi kutakiwa kuchukua tahadhari. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya habari Maelezo na kushoto ni  Mkurugenzi Msidizi Afya ya Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian Nkondo.02Mkurugenzi Msaidizi Afya ya Mimea,Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Fabian Nkondo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuwaelimisha wananchi kuhusu maboresho katika Sekta ya  Kilimo ili kuleta Tija.
………………………………………………………………………
Frank  Mvungi-Maelezo
Serikali imewatahadharisha wakulima nchini kuhusu uwezekano wa kutokea kwa viwavi jeshi katika msimu huu wa kilimo.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bw. Richard Kasuga wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza Bw. Kasuga amesema ili kuhakikisha kuwa kazi ya kukabiliana na viwavi jeshi inafanyika kwa umakini na ukamilifu wakulima kote nchini wanahimizwa kukagua mashamba yao mara kwa mara ili kubaini dalili za viwavi jeshi mapema hususani kwa mazao kama mahindi, mtama, uwele, ulezi, mpunga, ngano na shayiri .
Akifafanua zaidi Bw. Kasuga amesema ni vyema wakulima wanapaswa kutoa taarifa za awali pale wanapoona dalili za kuwepo kwa viwavi jeshi kwa kuwasiliana na Maafisa ugani na kuzingatia ushauri wa kitaalamu watakaopewa na kuupeleka kwa wakulima ambao ni walengwa.
Aliongeza kuwa Wakulima wamejengewa uwezo tangu 2008 ili kuweza kufanya utabiri kwa kuwapatia mafunzo na kusambaza mitego 374 ya utabiri wa viwavijeshi sambamba na vipima mvua katika vijiji vya mikoa ya ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dodoma, Lindi, Pwani na Mtwara.
Bw. Kasuga vilevile alisema  kuwa jumla ya lita 10,400 za viatilifu vya udhibiti wa viwavijeshi vilisambazwa katika Makao makuu ya Kanda  ambapo kanda ya Nyanda za juu Kusini (Mbeya) lita 2000, Kanda ya Magharibi (Shinyanga) lita 1000, Kanda ya Kati (Dodoma ) lita 4,000 Kanda ya Kaskazini (Arusha) lita 2000 na Kanda ya Mashariki Dar es salaam Lita 1,400.
Hadi mwezi Machi 2014 mlipuko ya viwavi jeshi imetokea na kudhibitiwa katika mikoa 9 ambayo ni Mtwara, Lindi, Pwani, Mbeya, Morogoro, Dodoma,Tanga, Arusha, na Kilimanjaro.
 Aidha Kasuga  alizitaka halmashauri za Wilaya kote nchini kufuatilia mtandao wa mitego ya utabiri katika ngazi ya vijiji na kuwahimiza watabiri wa vijiji husika kuendelea na kazi hiyo kwa msimu mzima wa kilimo.
Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika inaendelea na kazi ya kuratibu shughuli za kukabiliana na milipuliko ya viwavijeshi, kwelea kwelea, nzige na panya katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video