Wednesday, March 5, 2014

Baadhi ya majengo ya mradi huo yakiendelea na ujenzi.
Baadhi ya majengo ya mradi huo yakiendelea na ujenzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa Dege ECO Village wa Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu akifuatilia.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau akizungumzia kwa kifupi mradi wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau akizungumzia kwa kifupi mradi wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao ‘Dege ECO Village’ unaoendelea Kigamboni.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao ‘Dege ECO Village’ unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu) akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bodi ya NSSF kwenye jengo la mauzo ya nyumba za mradi wa Dege ECO Village, eneo hilo ndilo litakalokuwa likiendesha mauzo na taratibu zote za mradi baada ya kukamilika.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu) akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya NSSF jengo la mauzo ya nyumba za mradi wa Dege ECO Village, eneo hilo ndilo litakalokuwa likiendesha mauzo na taratibu zote za mradi baada ya kukamilika.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azimio, Mohamed Ikubal (mwenye kanzu) akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya NSSF jengo la mauzo ya nyumba za mradi wa Dege ECO Village, eneo hilo ndilo litakalokuwa likiendesha mauzo na taratibu zote za mradi baada ya kukamilika.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (katikati) akizungumza na viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF walipotembelea mradi wa ‘Dege ECO Village’ unaoendelea Kigamboni, utakao kuwa na nyumba bora na za kisasa eneo hilo.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao 'Dege ECO Village' unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
Viongozi mbalimbali wa NSSF pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa NSSF wakiangalia video ya muonekano wa ujenzi wa nyumba bora za kisasa ujulikanao ‘Dege ECO Village’ unaoendelea Kigamboni, utakavyo kuwa baada ya kukamilika.
WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) leo wametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa unaojulikana kwa jina la Dege ECO Village unaojengwa eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ujenzi huo wa mji wa kisasa ambao utakuwa na nyumba za kuishi za kisasa za watu wa kipato cha kati unajumuisha ujenzi wa nyumba zaidi ya 7,000 zikiwa na huduma zote za kujamii eneo moja.
Akizungumzia mradi huo mkubwa unaotekelezwa kati ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio, Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo aliwaeleza wajumbe wa Bodi ya shirika hilo kuwa ujenzi wa makazi hayo ya kisasa kwa wananchi wa kipato cha kati unaendelea vizuri.
Alisema eneo hilo litakuwa na nyumba bora na za kisasa zikiwa na huduma zote za msingi kwa jamii kama maduka, shule, hospitali, masoko, viwanja vya michezi, kituo cha polisi, kituo cha zimamoto, eneo la ujenzi wa majengo ya ibada, majengo ya burudani pamoja na miundombinu ya kisasa ya maji safi na maji taka.
Alisema ujenzi wa mradi huo wa kisasa utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuchukua watu takribani elfu 30 ambao watapata makazi bora nay a kisasa katika eneo hilo la Kigamboni.
Akifafanua zaidi Mhandisi Msemo alisema ujenzi wa nyumba hizo utakuwa na awamu tatu; ambapo awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2016 ikiwa na nyumba 2,500, huku awamu ya pili ya ujenzi itakamilika 2017 ikiwa na nyumba bora na za kisasa 2,500.
“…Awamu ya tatu tunatarajia ikamilike mwaka 2018 hii itakuwa na nyumba 2,460,” alisema Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Msemo akifafanua zaidi kwa waandishi wa habari juu ya mradi huo.
Aidha akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk. Ramadhan Dau alisema nyumba zote zitakazojengwa katika mradi huo zitauzwa kwa watu wenye kipato cha kati watakaohitaji. Alisema zipo zitakazouzwa kwa fedha taslimu na nyingine kwa makubaliano ya mikopo kadri ya utaratibu utakavyotolewa na shirika hilo pamoja na mwekezaji walieshirikiana naye kutekeleza mradi huo, yaani kampuni ya Azimio.
Alisema bei ya nyumba moja inakadiriwa kuuzwa kuanzia dola za Kimarekani elfu 80 hadi 130, na tayari wameanza kupokea fedha na maombi kwa watakaohitaji au kulipa kidogo kidogo kwa utaratibu utakao kubalika. Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa bodi walipongeza juhudi za uongozi wa NSSF kwa kubuni mradi huo wa kisasa ambao utawasaidia wengi na hivyo kushauri kuna haja ya kutekelezwa na mikoa mingine.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

0 comments:

voyeur porn porn movies sex videos hd porno video