Monday, March 3, 2014


Sarah  Kibonde Msika  ni  mkuu  wa mawasiliano  uhamasishaji  wa  mamlaka  ya usimamizi  na udhibiti  wa sekta  ya Hifadhi ya  jamii (SSRA) akizungumza na  wanahabari  hawapo pichani leo mjini Iringa 
Meneja wa NSSF  mkoa  wa Iringa Bw Marko Magheke akihojiwa na wanahabari  mjini Iringa leo 
Washiriki  wa  warsha  ya  NSSRA  wakiwa katika  ukumbi wa  warsha ukumbi wa VETA Iringa leo 
Sarah  Kibonde Msika  ni  mkuu  wa mawasiliano  uhamasishaji  wa  mamlaka  ya usimamizi  na udhibiti  wa sekta  ya Hifadhi ya  jamii (SSRA) wa pili kulia  akiwa wa wadau wengine  leo 
Wadau  mbali  mbali  wa warsha  hiyo ya  SSRA wakiwa katika ukumbi wa VETA leo 


Na Francis Godwin Blog 
WASHIRIKI  wa  warsha ya  siku  moja ya  mamlaka  ya  usimamizi   na udhibiti  wa sekta  ya Hifadhi ya  jamii  (SSRA) mkoani  Iringa  wamepongeza jitihada mbali  mbali  zinazoendelea kufanywa na SSRA katika kuwakutanisha   wadau  wa mifuko hiyo kwa  kuwapa elimu  zaidi.
 
Pongezi hizo zimetolewa  leo katika  ukumbi wa VETA mjini  Iringa na  washiriki wa  warsha hiyo  ambapo  wameshauri  mifuko  mingine ya  hifadhi ya jamii  kuiga mfano huo wa SSRA katika  kuwapatia  elimu  wanachama  wake  ili  kutojutia kujiunga na mifuko  hiyo.
 
Katibu  wa chama  cha  wafanyakazi  wa sekta ya  Kilimo  Bw  Deus Magesa  alisema  kuwa jitihada  kubwa  zimekuwa zikifanywa na SSRA  kwa  kuwatembelea  wadau  wake na  kuwapatia  elimu  mbali mbali juu ya  mifuko hiyo  pamoja na kupokea  changamoto mbali mbali  ila kwa mifuko husika ambayo  wanachama  wamekuwa wakikatwa  fedha  zao  imekuwa haina utaratibu wa kutoa  semina kwa wanachama  wake.
 
Hivyo  alisema  kuwa kama msimamizi mkuu  wa mifuko hiyo SSRA  amekuwa akifika  kutoa elimu iweje  mifuko  hiyo ya  kijamii kama NSSF  imekuwa  ikishindwa kufika  kutoa elimu kwa wanachama  wake  na kuwa  wanachama   wengi  bado wanajua  sheria  za  zamani ila  sheria mpya ya   mfuko huo hawaijui ila wahusika wa mfuko   huo wa NSSF  wamekuwa wakikaa kimya  .
 
“Mfuko  wa NSSF  kweli unachangamoto  nyingi kwa  wanachama   wake kwanza hawana kadi za uanachama  na   waajiri  wengi  wanatumia  sheria za  zamani kwa  mfanyakazi anapoingia
kuwa mwanachama  wa NSSF  ila mfumo huo bado  unamkwaza mwanachama …hivyo  nawaomba
NSSF   kuiga mfano wa SSRA katika  kutoa elimu na kuwabana   baadhi ya  maofisa wa NSSF ambao  wamekuwa wakitoa  lugha  chafu kwa  wanachama  wake”
 
Kwa  upande wake  meneja  wa NSSF  mkoa wa Iringa Marko Magheke  mbali ya  kupongeza jitihada za SSRA kwa  kuwafikia  wanachama  wake  bado alisema  kuwa  si kweli kama   NSSF imekuwa  ikiwanyanyasa   wanachama  wake na kuwa  kikwazo kikubwa cha kutoa  elimu  kinasababishwa na  waajiri  ambao  wamekuwa  hawataki  wafanyakazi  wao  kupewa  elimu  na  zaidi  maeneo ambayo elimu imetolewa basi ni  kupitia  vyama  vya  wafanyakazi wenyewe .
 
Kwani  alisema  ni vigumu   kuwakusanya  wafanyakazi  katika  kampuni  husika  bila ya  mwajiri  kukubali  kufanya  hivyo  na kuwa waajiri wengi hawapendi kuona  wafanyakazi wao  wanajua haki zao juu ya mifuko hiyo ya  kijamii.
 
“ Sisi  NSSF  kazi yetu moja  wapo ni  kutoa  elimu  kwa wanachama  ila tatizo ni waajiri wenyewe  ambao  wamekuwa  wakishindwa kutoa  ushirikiano  kwa  kuwatoa  wafanyakazi wake katika uzalishaji kwa nia ya  kupewa  semina”
 
Pia  alisema kuhusu  lugha  chafu kwa  wateja  yeye hajapata  kufikishiwa malalamiko  na  kuwa kila  mfanyakazi  wa NSSF  ananembo  inayoonyesha  jina  lake  hivyo kwa  yule  mteja atajibiwa vibaya  ni  vema kusoma jina na  kupeleka  malalamiko  yake kwa meneja.
 
Hata  hivyo  aliwataka  waajiri  wote  kuhakikisha wanafikisha michango ya wanachama  wao kwa wakati  na  kuwa mwajiri  kutofikisha michango hiyo ni  kinyume na  taratibu na NSSF  inawez kuchukua hatua kali dhidi yake.
 
Alisema  kumekuwepo na  changamoto kubwa  ya  waajiri kutofikisha  michango ya  wanachama na  kuwa  eneo  moja wapo linalosumbua kwa  waajiri wake  kutofikisha  michango ya  wanachama wake ni pamoja na  vyombo  vya  habari  ambapo  katika  mkoa wa Iringa  wadaiwa sugu ambao wamepata  kufikishwa mahakamani ni  pamoja na  kituo kimoja  cha radio mjini hapa na sekta  nyingine  mbili.
 
Sarah  Kibonde Msika  ni  mkuu  wa mawasiliano  uhamasishaji  wa  mamlaka  ya usimamizi
na udhibiti  wa sekta  ya Hifadhi ya  jamii (SSRA) nchini  alisema  kuwa  lengo  la  kufika  mkoani  Iringa ni  kuhamasisha  wafanyakazi  kuijua mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii.
 
Kwani  lisema kuwa wakati takwimu  zinaonyesha   kuwa  watanzania  kama  milioni 45  na nguvu kazi kama  milioni 22 ila wanachama waliojiunga na mifuko hilo ni milioni 1.7 pekee  hivyo  lengo la SSRA ni  kuona  wanachama  wanaongezeka  zaidi.
 
Aliitaja  mifuko  hiyo ya  hifadhi ya jamii  kwa Tanzania  bara  kuwa ni mfuko wa  hifadhi ya  jamii  (NSSF),Mfuko  wa pensheni wa PPF,mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma  (PSPF),,mfuko wa
pensheni kwa  wafanyakazi wa serikali (GEPF),mfuko  wa Pensheni wa LAPF na mfuko wa Taifa  wa bima  ya Afya  (NHIF) na  kuwa  kila mtanzania  anapaswa kujiunga na moja kati ya mifuko   hiyo.
 
Alisema  kuwa  mifuko hiyo sita  inasimamiwa na SSRA na  kuwa lengo  ni kuona  wanachama  wake
wanaendelea  kujiunga kwa  wingi na kunufaika  na mifuko hiyo.
 
Msika  alisema  kuwa  Hifadhi ya  jamii  ni haki  ya  kila  mtu  na  hii imeainishwa  katika  ibara   ya 11(1)) ya katiba  ya jamuhuri ya Muungano WA Tanzania  na  sera ya  Taifa  ya Hifadhi  ya jamii   ya mwaka 2003 na  kuwa haki  hiyo  pia   imeainishwa kwenye  mkataba  wa kimataifa  wa  haki  za binadamu  wa mwaka 1948 pamoja  na mikataba   ya  shirika  la kazi  Duniani  (ILO).

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video