Thursday, March 27, 2014

P1040522 copyMkurugenzi na muasisi wa taasisi ya Tanzania Street Children(TSC),Atlaf Hirani akimkabidhi vifaa vya jezi meneja msafara wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania,Majuto Ismail juzi jijini Mwanza kabla ya kuondoka nchini kuelekea nchini Brazil kushiriki michuano ya kombe la dunia la watoto wa mitaani(picha na moses mashalla)
……………………………………………………………
Mahmoud Ahmad,Mwanza 
Vijana kutoka kituo cha kukuza vipaji vya  watoto wa mitaani cha TSC Sports Academy kilichopo jijini Mwanza wanataraji kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya soka ya kombe la dunia la watoto wa mitaani itakayoanza kutimua vumbi kuanzia machi 30 mwaka huu nchini Brazil . 
Tanzania kwenye mashindano hayo itashiriki michuano hiyo kwa wavulana tu ambapo timu hiyo itaondoka machi 27 kuelekea mjini Rio De Janeiro nchini Brazil .
Ambapo mashindano hayo yatazikutanisha timu 15 za wavulana na timu 10 za wasichana kutoka mataifa mbalimbali duniani.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na mkurugenzi na mwanzilishi wa TSC Sports Academy,Altaf Hiran wakati akigawa vifaa mbalimbali kwa ajili ya timu itakayoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo  alisema kuwa mashindano hayo yatawakutanisha zaidi ya vijana 250 .
 
Alisema kuwa vijana hao ni kati ya umri wa miaka U 15 na U 17 yakiwa ni utangulizi wa fainali za kombe la dunia la FIFA linalotaraji kutimua vumbi nchini Brazil mwaka huu.
 
Hiran,ambaye ataongoza msafara wa timu hiyo alisema kuwa mashindano hayo yatachezwa  katika mji wa Rio De Janeiro na kumalizika Aprili 9 mwaka huu. 
Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo ya kombe la dunia la watoto wa mitaani ambapo mara ya kwanza ilishiriki nchini Afrika kusini mwaka 2010 na kufanikiwa kushika nafasi ya pili baada ya kuondolewa katika fainali kupitia mikwaju ya penati na India .
Timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu zimepangwa katika makundi matatu ya awali kwa wavulana na wasichana ambapo Tanzania iko katika kundi B pamoja na timju za Burundi, Argentina , Nicaragua na Ufilipino upande wa wavulana. Huku katika kundi A la wavulana lina timu za Afrika Kusini,Liberia,Misri,Indonesia na wenyeji  Brazil na kundi C lina timu za Mauritius,Kenya,Marekani,India na Pakistan.
 
Kwa upande wa wasichana kundi A kuna timu za Zimbabwe,Indonesia, na wenyeji Brazil wakati kundi B kuna timu za Afrika Kusini,Ufilipino, na El Salvador wakati kundi C kuna timu za Msumbiji,Nicaragua na Uingereza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video