Afisa habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya nakala ya maombi ya ajira isiyokidhi vigezo hali inayosababisha waombaji wengi wenye sifa kushindwa kupata ajira Serikalini. Kulia ni Afisa Habari Idara ya Habari Maelezo Frank Mvungi na kushoto ni Afisa Udhibiti na Ubora wa Sekretarieti hiyo bw. Chistopher Liganga.Afisa habari Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma Bi Riziki Abrahamu akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu waombaji kazi kujiandaa vyema ili kukidhi vigezo vya usaili, na kushoto ni Afisa Udhibiti na Ubora wa Sekretarieti hiyo bw. Chistopher Liganga.
…………………………………………………………………………
Frank Mvungi-Maelezo
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuandaa programu ya Elimu kwa umma ili kuwawezesha waombaji wa kazi kuweza kutimiza vigezo vinavyohitajika ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata kazi walizooomba.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira Bi Riziki Abraham wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Bi Riziki amesema mpango huo unalenga kuwajengea uwezo waombaji wa ajira kuweza kuandaa wasifu wao vyema (CV), kuandika barua za maombi kwa ufasaha, kuwajengea uezo wa kufanya maandalizi sahihi kabla ya usaili.
Aliongeza kuwa hali hiyo inatokana na kujitokeza kwa changamoto za wahitimu walio wengi kushindwa kutimiza vigezo husika ili waweze kupata ajira wanazoomba.
Bi Riziki alisisitiza na kusema kuwa katika kutekeleza mpango huo watashirikiana na Taasisi za Elimu hapa nchini ili kuwasaidia wanafunzi wanaohitimu vyuoni ili kuwajengea uwezo ili waweze kukidhi vigezo mara wanapoomba ajira Serikalini.
Katika kipindi cha miaka mine Tangu kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa umma imekabiliana na changamoto nyingi ikiwemo ubora wa wahitimu wanaowasilisha maombi ya kazi Serikalini kuanzia ngazi ya Sekondari, Astashahada ya juu, Shahada ya uzamili pamoja na shahada ya uzamivu.
Pia Bi Riziki alibainisha kuwa katika tathmini sekretarieti kupitia maombi ya ajira yaliyowasilishwa wamebaini mapungufu yatokanayo na ubora hafifu wa baadhi ya wahitimu wanaoomba kazi kupitia chombo hiki.
Dhana potofu ya wahitimu kuwa kuwa na vyeti pekee ndicho kigezo pekee cha mhitimu kupata ajira badala ya kuwa na uelewa mpana wa kile walichoombea kazi,kutotilia maanani sifa na masharti ya Tangazo husika, kutojiamini,kukosa uzoefu wa kazi inayohitaji uzoefu na uwezo mdogo wakutumia lugha kwa ufasaha.
0 comments:
Post a Comment